Mshambuliaji
wa Chelsea na timu ya taifa ya Cameroon Samuel Eto’o ambaye alikuwa
mmoja wa wafungaji wa mabao mawili ya Chelsea yaliyowaondoa Galatasary
katika michuano ya UEFA Champions League jumanne iliyopita amepost picha
kwenye mtandao wa Instagram akiwa pamoja na mshambuliaji Didier Drogba –
ambaye amekuwa mpinzani wake kwa muda mrefu katika medani za soka
barani Afrika.
Eto’o alipost picha akiwa na Drogba na kuandika ujumbe wa kuonyesha
uimara wa mahusiano yao pamoja na kuwa na upinzani kwenye soka.
Eto’o aliandika kifaransa: “Deux enfants d’une meme mère,…Mama Africa!!!”
Ambapo tafsiri yake ni “Watoto wa mama mmoja….Mama Africa!”
Post a Comment