Wakati mamilioni ya mashabiki wa timu hiyo wakisubiri ratiba, gwiji wa soka na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Dwight Yorke amezitaja timu 3 ambazo kama ikitokea moja wapo ikapangwa kucheza na United katika hatua ijayo ya ligi ya mabingwa ulaya, basi timu yake ya zamani itapata matokeo chanya.
Yorke amezitaja timu za Atletico Madrid, Borrusia Dortmund na PSG – kwamba kati ya timu yoyote kati hizo, ikitokea mojawapo imepangwa kucheza na United basi klabu yake ya zamani itapata matokeo ya ushindi na kwenda kucheza hatua ya nusu fainali ya Champions league.
Pia amezitaja Real Madrid, Barcelona na Bayern Munich kuwa ndio timu ambazo asingependa wakipangwa nazo katika hatua ijayo ya michuano hiyo.
VIDEO ZA YORKE AKIONGELEA SUALA HILO


Post a Comment