WAKINAMAMA WAKIWA NA HUZUNI BAADA YA KUSIKIA MWANAMKE ALIYEFANYIWA UKATILI
AFISA WA TAKUKURU MKOANI MARA AKITOA MSAADA KWA MWANAMKE ALIYEFANYIWA UKATILI
FEDHA ZILIZOCHANGWA KUMSAIDIA MWANAMKE ALIYEFANYIWA UKATILI
MENEJA
KITENGO CHA MAENDELEO YA KANISA LA ANGLICANA JIMBO LA MARA DOCTA
THEOPHIR KAYOMBO PIA ALIGUSWA NA MWANAMKE HUYO NA KUCHANGIA
KATIBU
TAWALA WA MKOA WA MARA BENEDICT OLE KUYAN AKIMPA MCHANGO WA FEDHA
ZILIZOCHANGWA MWANAMKE ALIYEFANYIWA UKATILI MJINI BUNDA
KANISA la
Anglicana Jimbo la Mara kupitia Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
wameahidi kusaidia kuchangia gharama za matibabu za Sumayi Girandi
ambaye ni Mwanamke aliyefanyiwa ukatili wa kukatwa mkono na sehemu za
siri na aliyedaiwa kuwa ni mume wake.
Meneja
mradi wa Maendeleo ya Jamii wa Kanisa hilo docta Theophir Kayombo alitoa
ahadi hiyo siku chache baada ya Mwanamke huyo kutoa ushuhuda wake
katika maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani iliyofanyika kimkoa
wilayani Bunda.
Alisema
Kanisa liliguswa na ukatili mbaya aliofanyiwa Mwanamke huyo kwa kufuatwa
nyumbani kwake usiku akiwa na watoto wake na kuanza kukatwa sehemu
mbalimbali za mwili wake na kupelekea kupoteza mkono wake mmoja wa
kushoto na kuharibiwa jicho.
Kayombo
alisema kutokana na rufaa aliyopewa Mwanamke huyo ya kwenda hospitali ya
(KCMC) iliyopo Moshi Kanisa litatoa msaada wa karibu kuhakikisha
anakwenda kufanyiwa matibabu ya kina ili kurekebisha jicho ambalo
limeharibiwa na kumsababishia maumivu.
Alisema
wameguswa na ukatili mbaya aliofanyiwa na kuona kuna umuhimu mkubwa kama
sehemu ya jamii kuhakikisha wanakuwa karibu na muhanga huyo ili kutoa
mchango wao katika kusaidia tatizo.
"Kwanza
tunalaani ukatili huu aliofanyiwa Sumayi kwa kuvamiwa akiwa nyumbani
kwake na huyo aliyekuwa mume wake na kushambuliwa vibaya kwa mapanga na
kupoteza mkono wake wa kushoto na kuharibiwa jicho moja.
"Licha ya
kupoteza mkono tulimsikia kwenye ushuhuda wake yakwamba aliandikiwa
rufaa ya kwenda (KCMC)tutasaidia suala hilo lakini tunaaiomba jamii
ibadilike na kuachana na matukio ya ukatili ambayo yanapoteza nguvu kazi
ya Taifa.
Akitoa
ushuhuda wa tukio hilo la kufanyiwa ukatili katika maazimisho ya siku ya
Wanawake duniani mjini Bunda,Sumayi Girandi alisema usiku wa julai 4
mwaka 2013 akiwa nyumbani kwake katika Kijiji cha Kunzugu wilayani Bunda
alivamiwa na aliyekuwa mume wake kabla ya kutengana na kumkata kwa
mapanga.
Alisema
aliyekuwa mume wake waliyetengana kutokana na tabia akiwa na mwenzake
walimvamia ndani ya nyumba yake na kumkata sehemu mbalimbali za mwili
wake na kupoteza mkono wa kushoto huku jicho moja likiwa limeharibiwa
vibaya.
Sumayi
alisema baada ya kupata matibabu katika hospitali ya DDH Bunda
aliandikiwa rufaa ya kwenda (KCMC) kwa ajili ya oparesheni ya jicho
linalomsumbua na kuwaomba wananchi kuweza kumsaidia ili kwenda kupata
matibabu zaidi.HABARI NA SHOMARI BINDA
Post a Comment