Tukio
hilo limetokea usiku wa kuamkia Machi 17 mwaka huu majira ya saa 7
usiku, ambapo mtuhumiwa aitwaye Yohana Sanga alimchoma kisu kifuani
baada ya kumfumania akiwa na mpenzi wake(hawara) aliyetambulika kwa jina
la Matilda Sanga ambaye pia ni mkazi wa kijiji hicho cha Mago
Imeelezwa
kuwa siku ya tukio marehemu ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na
Bi. Matilda, waliongozana usiku hadi nyumbani kwa mwanamke huyo kwa
ajili ya kulala pamoja, na ndipo mtuhumiwa ambaye ni Yohana, ambaye
inadaiwa alikuwa akifuatilia nyendo zao aliwavamia nyumbani kwa mwanamke
huyo na kumchoma kisu kifuani marehemu hadi akapoteza maisha
Baada
ya mtuhumiwa kutenda mauaji hayo katika nyumba ya huyo hawara yake
alichomoa kisu hicho na kumshikisha marehemu mkononi, kwa lengo la
kupoteza ushaidi ili ionekane kuwa alijiua mwenyewe
Akizungumzia
tukio hilo Afisa upelelezi wa polisi wilaya ya Makete ambaye pia ni
Kaimu OCD wilaya ya Makete, Mrakibu wa polisi Gosbert Komba amesema wao
kama jeshi la polisi walipewa taarifa
na Bw. Emannuel Sanga (25) ambaye
aligundua kuuawa kwa marehemu Frenk na wao kama polisi walifuka eneo la
tukio na kuthibitisha mauaji hayo
Bw.
Komba amesema mtuhumiwa wa mauaji hayo amekimbia mara baada ya tukio na
jeshi hilo linamtafuta na kutoa wito kwa wananchi kwa kuwa mtuhumiwa
anafahamika watoe taarifa polisi endapo watamuona ili atiwe mbaroni
Amesema
kwa sasa wanamshikilia mwanamke huyo kwa mahojiano zaidi kuhusiana na
tukio hilo, na katika mahojiano na jeshi hilo mwanamke huyo amesema
alishaachana na Yohana ambaye ni mtuhumiwa aliyetenda mauaji hayo na kwa
sasa mapenzi yake yalikuwa kwa marehemu Frenk
"Kwa
kawaida huyu mwanamke aligonganisha magari (aligonganisha wapenzi), na
sisi kama polisi tunatoa wito kwa hawa dada zetu au wanawake, kuwa na
mpenzi mmoja, lakini pia watu wasijichukulie sheria mkononi" alisema
Komba
Wakizungumza
na mwandishi wetu baada ya kumzika marehemu hii leo, baadhi ya wananchi
ambao wametaka majina yao yahifadhiwe wamesema, mwanamke huyo alikuwa
na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wote wawili kwa wakati mmoja jambo
lililosababisha kifo Frenk
Wamesema
licha ya mauaji hayo kutokea usiku na mwanamke huyo kushuhudia,
hakupiga kelele za kuomba msaada wala kutoa taarifa kwa majirani bali
alikaa kimya hadi wapita njia walipogundua mauaji hayo jana jambo
linalowapa wasiwasi wananchi hao kuwa huwenda mwanamke huyo anafahamu
kilichokuwa kikiendelea.
Post a Comment