NAIBU WAZIRI WA FEDHA MH:MWIGULU
LAMECK NCHEMBA ZIARANI NCHINI UFARANSA NA UJERUMANI KUHUDHURIA MKUTANO
WA ACP NA DEVELOPMENT COOPERATION FORUM
Naibu Waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Lameck
Nchemba ameanza ziara yake ya Kikazi Nchini Ufaransa kwa Muda wa Siku
mbili (Tar.18 na 19/03/2014) atakapo hudhuria Mkutano wa Umoja wa Nchi
za Africa,Caribbean na Pacific.Mkutano huo ni Miongoni mwa Mikutano
ilinayofanyika Kila Mwaka ya
Umoja huo.Kwenye Mkutano huo Mh.Mwigulu Nchemba natarajia Kushiriki Mjadiliano ya namna ya Kuzijengea Uwezo madhubuti Nchi zinazoendelea katika Maswala ya Biashara na Uwekezaji.Pia watafanya tathimini ya Utekelezaji wa Mikakati ya Maendeleo waliokuwa Wamejiwekea Mwaka 2013.

Baada ya Ufaransa,Mh.Mwigulu Nchemba
ataelekea Nchini Ujerumani kuhudhuria Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano
wa Maendeleo (Development Cooperation Forum),Mkutano utakao husisha Nchi
zilizoendelea,Zinazoendelea na Taasisi Kubwa za Kifedha na Maendeleo
Duniani.
Katika Mkutano huu wa Ujerumani,Washiriki watajadiliana namna Misaada inayotolewa inavyotumika Kwenye Shuguli zilizolengwa za Maendeleo na Vile Vile Utekelezaji wa ahadi za Utoaji wa Misaada kutoka Nchi zilizoendelea katika hali ya Uwazi.

Naibu Waziri wa Fedha atakuwepo Ujerumani kwa Muda wa Siku mbili(Tar.20 na 21/03/2014).
Mungu Ibariki Tanzania.
Post a Comment