Stori: Mwandishi Wetu, KAHAMA
MWANAFUNZI wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Majengo, Kahama mkoani Shinyanga, Said Siraji (13) anaendelea vizuri katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama alikolazwa baada ya kunusurika kifo kwa kuchinjwa shingoni na baba yake mzazi kwa madai ya kushindwa kumtibu mtoto huyo kwa matatizo yake ya afya.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dokta Joseph Fwoma alisema Said anaendelea vizuri baada ya kufikishwa hospitalini hapo alfajiri ya Machi 6, mwaka huu baada kuokotwa na wasamaria wema akiwa anakimbia huku akivuja damu shingoni.
Dokta Fwoma alisema walimfanyia upasuaji na kumshona sehemu ya koromeo aliyochinjwa na hadi alasiri ya siku hiyo, hali yake ilikuwa ikiendelea vizuri alipoongezewa damu.
Naye mama mzazi wa Said, Mariamu Idd (35), alisema siku moja kabla ya tukio, baba mzazi wa mtoto huyo, Siraji Salvatory,45, (waliachana) alikwenda kwake Majengo na kumchukua.
Mama huyo alisema asubuhi iliyofuata alishtuka sana kupigiwa simu na nduguye mmoja akielezwa mtoto wake amechinjwa na aliyehusuka ni baba yake mzazi.
“Kwa kweli nilishtuka sana, tena sana. Mwanangu angekufa maana baada ya kumchinja koromeo baba yake aliamini ameshammaliza akamwacha porini kisha yeye akakimbilia Kituo cha Polisi Kahama kujisalimisha (hadi sasa anashikiliwa kituoni hapo).
Mariam alisema, awali Salvatory alikuwa akimchukua Said na kwenda naye nyumbani kwake Malunga baada ya siku kadhaa alimrudisha akidai amechoshwa na gharama za matibabu kutokana na mtoto huyo kuwa na matatizo ya kiafya (hakuyasema).
Jeshi la Polisi wilayani Kahakama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Mtoto
Said Siraji akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama alikolazwa baada
ya kunusurika kifo kwa kuchinjwa shingoni na baba yake mzazi.

Post a Comment