Viatu vipya: Gareth Bale atavaa viatu vyake vipya kutoka kampuni ya adidas
MCHEZAJI
ghali zaidi duniani, Gareth Bale kesho katika mchezo wa marudiano wa
ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Schalke 04 dimba la Santiago
Bernabeu atavaa viatu vipya `njumu` kutoka kampuni ya Adidas.
Viatu hivyo vya `adidas F50 crazylight`, vina uzito wa gramu 135 na vimebuniwa kwa ufundi mkubwa.
Gareth
Bale alionekana leo hii akijaribu viatu hivyo kwenye vyumba vya
kubadilishia nguo wakati wa mazoezi ya Real Madrid na atakuwa wa
kwanza pekee kuvaa viatu hivyo.
Nyota huyo raia wa Wales atavitumia kesho dhidi ya
Schalke uwanja wa Bernabeu.
"Nimevijaribu
viatu hivi kwenye mazoezi na nimejisikia vizuri". Alisema Bale ambaye
ameandika kwenye akaunti yake ya Twita kuwa atatumia viatu vipya.
"Ni viatu vyepesi sana na vitanipa faida kubwa katika uchezaji wangu". Alisema
Post a Comment