Mtu mmoja
amekufa papo hapo na wengine 22 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la
kampuni ya saibaba walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Dar es salaam
kwenda Kyela mkoani Mbeya kupinduka katika kijiji cha Mwambegele
wilayani Rungwe.
Safari ya
basi la kampuni ya Saibaba lenye namba za usajili T 973 AVW kutoka
jijini Dar es Salaam kwenda wilayani Kyela imeishia kwenye kona kali ya
Mwambegele wilayani Rungwe, baada ya basi hilo kupinduka, ambapo mkuu wa
wilaya Rungwe Crispine Meela ni miongoni mwa watu ambao wamewahi kufika
kwenye eneo la tukio na hapa anaelezea chanzo cha ajali hiyo.
Baadhi ya
majeruhi wa ajali hiyo ambao wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya
Rungwe, makandana, wamesema mwendo kasi wa basi hilo ndio ambao
umewasababishia ajali ambayo imesababisha kifo cha dereva wa basi hilo.
Mganga
mkuu wa hospitali ya wilaya ya Rungwe, Mandana, Stanford Mwakatage
amethibitisha kupokea mwili wa mtu mmoja na majeruhi 22 wa ajali hiyo
huku akisema kuwa baadhi ya majeruhi hali zao bado sio za kuridhisha
Post a Comment