Mkurugenzi
Msaidizi wa Habari, elimu na mawasiliano wa bodi ya mikopo Tanzania,
Cosmas Mwaisobwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana
kuhusiana na masuala ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
nchini. Pamoja nae ni Ofisa Mwandamizi Habari, elimu na mawasiliano, Veneranda Malima.
*********
1.0 UTANGULIZI
Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilianzishwa kwa sheria Na. 9 ya
mwaka 2004 na kuanza rasmi majukumu yake Julai 2005. Bodi ina majukumu
makuu mawili; kwanza ni kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji
waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu kwa ajili ya masomo ya
Shahada au Stashahada ya juu. Jukumu la pili ni kukusanya marejesho ya mikopo iliyotolewa kwa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu tangu
mwaka 1994.
Tangu
kuanzishwa kwake, Bodi imefanikiwa kutoa mikopo kwa idadi kubwa ya
Wanafunzi ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla Bodi haijaanzishwa.
Mwaka 2005/2006 Bodi ilipoanza kazi ilitoa mikopo kwa Wanafunzi 42,729
wa elimu ya juu kwa kutumia bajeti shilingi Bilioni 56.1.
Idadi
ya Wanafunzi wa elimu ya juu wanaopewa mikopo imeendelea kuongezeka
kutoka wanafunzi 42,729 mwaka 2005/2006 hadi Wanafunzi 97,348 mwaka
2012/2013. Hii ni sawa na ongezeko la wastani wa 10.4%
kwa mwaka. Mikopo iliyotolewa kwa Wanafunzi wahitaji iliongezeka kutoka TZS 56.1 Bilioni mwaka 2005/2006 hadi TZS 306 Bilioni mwaka wa fedha 2012/2013.
kwa mwaka. Mikopo iliyotolewa kwa Wanafunzi wahitaji iliongezeka kutoka TZS 56.1 Bilioni mwaka 2005/2006 hadi TZS 306 Bilioni mwaka wa fedha 2012/2013.
Kwa
mwaka wa masomo 2013/2014, jumla ya wanafunzi 95,178 wamenufaika na
mikopo hadi kufikia tarehe 15 Machi, 2014 ambao mikopo ya kiasi cha TZS
223,977,042,853.00 imekwishalipwa.
Mwaka
|
Idadi
ya Wanafunzi Waliokopeshwa |
Ongezeko
(%)
|
Kiasi
kilichoko-peshwa
(Tshs
Bilioni) |
Ongezeko
(%)
|
2004/05 (Na
Wizara) |
16,345
|
-
|
9.9
|
-
|
2005/2006
|
42,729
|
161.4
|
56.1
|
467
|
2006/2007
|
47,554
|
11.3
|
76.1
|
35.7
|
2007/2008
|
55,687
|
17.1
|
110.8
|
45.6
|
2008/2009
|
58,798
|
5.6
|
139.0
|
25.5
|
2009/2010
|
72,035
|
18.4
|
237.8
|
28.7
|
2010/2011
|
92,791
|
28.8
|
230.0
|
24.5
|
2011/2012
|
94,533
|
2.0
|
311
|
35.0
|
2012/2013
|
97,348
|
2.9
|
335.2
|
7.2
|
Post a Comment