Bondia
wa ngumi za kulipwa Fadhili awadh amefariki dunia katika hospital ya
Mwananyamala jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa siku kadhaa.
Marehemu Fadhili Awadh alikuwa ni miongoni mwa mabondia waliochaguliwa kucheza mpambano
wa ubingwa tarehe 29 mwezi huu wa tatu dhidi ya mpinzani wake toka
Tanga Alan Kamote, na alikuwa katika maandalizi ya mpambano huo.
Sababu
ya kifo chake kwa ripoti ya daktari wa Mwananyamala kwa kiongozi wa
ngumi Ibrahim Kamwe ni kuwa fadhili alikuwa na malaria na alitumia dozi
ya metakelfin, na hali ilibadirika pale alipojaribu kufanya mazoezi
na kujisikia vibaya na kuwahishwa katika hospitali hiyo ambayo alikaa
kwa siku mbili akiendelea na matibabu na hatimae umauti ulipomkuta.
Fadhili
awadh mwenye umri wa maika 32 alikuwa anaendelea vizuri katika mchezo
huo kiasi cha kufikia kucheza pambano la ubingwa katika ukumbi wa PTA
sabsaba, akiwasindikiza mabondia Japhet Kaseba na Thomas Mashali.
Shughuli za maazishi zinafanyika nyumbani kwao maeneo ya manzese.
Sisi tulimpenda lakini Mungu alimpenda zaidi,
Ailaze roho ya marehemu Fadhili awadh “Tiger” peponi
AMINA
Post a Comment