Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BREAKING NEWWZZZZ: MBUNGE WA CHADEMA AKAMATWA NA JESHI LA POLISI IRINGA AKITUHUMIWA KUGAWA FEDHA KWA WANANCHI








Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa,Bi.Jesca Msavatavangu akizungumza na wanahabari jioni ya leo mara baada ya tukio hilo la kukamatwa kwa Mbunge wa CHADEMA akigawa fedha kwa wanakijiji siku moja kabla ya uchaguzi kufanyika.Uchaguzi wa Jimbo hilo unatarajiwa kufanyika kesho siku ya jumapili,ambapo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura.


 Ikiwa imebaki siku moja kabla ya uchaguzi Mdogo wa Ubunge jimbo la Kalenga,Iringa Vijijini,Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili amekamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini akigawa Fedha kwa wanakijiji hao,akijua fika Wananchi hao wanatarajiwa kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya jumapili.


Pichani shoto ni Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili akielekezwa sehemu ya kupita wakati wakiondoka ofisi za makao makuu ya CCM mjini Iringa jioni ya leo,akituhumiwa kukutwa akigawa fedha kwa Wanakijiji wa Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini,ambapo Wananchi hao wanatarajiwa kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya jumapili.


 Mbunge huyo wa Chadema akipakizwa kwenye gari tayari kupelekwa kituo cha Polisi kwa taratibu nyingine za kisheria.


Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili akiwa ndani ya gari ya polisi mara baada ya kukakamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini akituhumiwa kugawa Fedha kwa wanakijiji 




Gari ya Polisi PT 1895 ikiondoka na mtuhumiwa huyo,mara baada ya kuchukuliwa kwenye makao Makuu ya chama cha CCM alikokuwa ameshikiliwa na uongozi wa chama hicho,kwa taratibu nyingine za kisheria.


Baada tu ya kukamatwa live akitoa rushwa!! Mbunge Rose Kamili wa Chadema!
credit: michuzijr blog
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top