NIMECOPY NA KUATTACH taarifa yangu ya Pingamizi dhidi ya mgombea wa CHADEMA hapa chalinze....;;...
Fabian L. Skauki
TAARIFA YA PINGAMIZI LA MGOMBEA WA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE .
FABIAN LEONARD SKAUKI – MGOMBEA CHAMA CHA WANANCHI –CUF
DHIDI YA
MATHAYO MANG’UNDA TORONGEY – MGOMBEA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO -CHADEMA
13.03.2014
Mimi FABIAN
L. SKAUKI, mgombea ubunge wa uchaguzi mdogo jimbo la CHALINZE kwa
Ticket ya THE CIVIC UNITED FRONT (CUF) ninamwekea Pingamizi mgombea wa
chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwamba amepoteza sifa za
kuwa mgombea kwa sababu zifuatazo.
1. Ndugu
MATHAYO. M. TORONGEY amejaza Taarifa za uongo kwenye Fomu yake kwamba
kazi anayoifanya ni BIASHARA. Sio kweli, kwa sababu hajaweka vielelezo
vya yeye kufanya hiyo kazi. Hajulikani anafanya kazi gani.
2. Ndugu
MATHAYO .M. TORONGEY amejaza katika fomu kwamba anajua kusoma na
kuandika Kiswahili na kiingereza. Taarifa hizi ni za uongo, mgombea huyu
hajui kusoma wala kuandika Kiswahili wala kiingereza, na kwamba
amedanganya na amepoteza sifa za kuwa mgombea.
3. Ndugu
MATHAYO .M.TORONGEY amedanganya kwa kughushi/kufoji sahihi za
wadhamini,ambao amewaorodhesha kwenye fomu ya kuomba kuthibitishwa kuwa
mgombea. Ambapo katika fomu hizo wadhamini wote sahihi zao zimefojiwa na
hazifanani na zile zilizokuwepo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura
na kwamba sahihi zote hizi zimesainiwa na mtu mmoja ambaye sio
muhusika. Hivyo anapoteza sifa ya kuendelea kuwa mgombea.
4. Ndugu
MATHAYO.M.TORONGEY ameshindwa kutimiza mahitaji ya kisheria ya kuwa na
wadhamini wasiopungua 25, badala yake amedhaminiwa na wadhamini 28 ambao
kati yao wadhamini 7 sio wapiga kura halali wa jimbo la CHALINZE, na
kwamba Taarifa zao na namba zilizojazwa hazifanani.
Hivyo anabakiwa na wadhamini halali 21 ambao kisheria hawatoshi kutimiza matakwa ya kisheria.
Majina ya wadhamini hao ambao hawakidhi matakwa ya kisheria na namba zao ni
JINA LA MDHAMINI NAMBA YA KADI KURA
1. HABIBU ALLY SAIDI * 16886275*
2. MOHAMMED RAMADHANI *30376567*
3. ABDULKADIR ALLY *49264905*
4. SHABANI SULEYMAN *16984045*
5. JUMA MRISHO *48759563*
6. RAJABU ALLY *16872368*
7. MANENO MIRAJI *16872059*
Wananchi
wenye namba na majina hayo hapo juu waliojazwa kama wadhamini kuanzia
namba 1 hadi 7 kwenye fomu yake hawana sifa za kupiga kura kwenye maeneo
ambayo wamejazwa wanatokea.
Hii
ni kutokana na ukweli kwamba idadi halali ya wadhamini wanaobaki
ukiwaondoa hao saba watabaki 21, hawakizi vigezo vya kuwa wadhamini.
5. Ndugu
MATHAYO.M.TORONGEY amedanganya Uraia wake, na kwamba yeye si
Mtanzania wa kuzaliwa ndio maana hana vielelezo halali vinavyohusu uraia
wake. Hivyo anakosa sifa ya kuwa mgombea.
Hivyo
ninaomba Tume ya Uchaguzi kutengua uteuzi wa mgombea wa chama cha
demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ndugu MATHAYO.M.TORONGEY kwa kuwa
anakosa sifa za yeye kuendelea kuwa mgombea.
Wako katika ujenzi wa Taifa
FABIAN LEONARD SKAUKI
*********************************
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE.
THE CIVIC UNITED FRONT
+255 786 189 070/+255 754 849 450
Post a Comment