Wawakilishi
pekee wa Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika,
Dar Young Africans tayari wameenda mjini Alexandria kujiandaa na mchezo
wa kesho katika Uwanja wa Border Guard stadium (Haras el Hadod) dhidi ya
mabingwa watetezi wa klabu bingwa Afrika, National Al Ahly ya Misri.
Kuelekea
katika mchezo huo, kocha wa Yanga, Hans Van Pluijm amesema lazima Yanga
leo hii waupime uwanja huo kwa kufanya mazoezi mepesi kabla ya mtanange
wa kesho.
Kocha
huyo Raia wa Uholanzi alisema kikosi chake kipo imara na matarajio ya
benchi la ufundi ni kuwatoa waarabu hao ambao walifungwa bao 1-0, katika
mchezo wa kwanza uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, machi mosi mwaka
huu.
Bao hilo pekee lilitiwa kambani na beki wa kati na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub `Canavaro` katika dakika ya 82.
Post a Comment