Hii
ni kampeni ya Rose Ndauka ambayo kaipa jina la Ng’arisha Tanzania
inayohamasisha kuweka jiji la Dar es salaam katika hali ya usafi na
kupendeza ambapo kampeni hii inahusisha kufagia baadhi ya mitaa katika
manispaa ILALA ili kuzoa taka na kuzitupa maeneo husika.
Kampeni ilianza majira ya saa moja asubuhi na kumalizika saa 3
asubuhi baada ya hapo ukafanyika uzinduzi wa jiko la kuchomea taka mtaa
wa Lumumba katika Manispaa ya Ilala ikiwa ni kama ishara ya kuhamasisha
raia wote Kuamka na Kubadilika na kuonyesha mapenzi kwa kuweka miji
katika hali safi kwa kusafisha maeneo wanayoishi.
Hizi ni baadhi ya picha za mastar mbalimbali wa Tanzania walivyojumuika na Rose Ndauka katika kampeni hii.
Meya wa Ilala Jerry Silaa.
Post a Comment