Kamanda
wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam nchini Tanzania, Suleiman Kova,
akizungumza wakati wa sherehe ya kuwazawadia vyeti vya sifa na zawadi
kwa polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam wapatao 127 ambapo kati ya
hapo Maofisa 6, Wakaguzi 8, S/Sgt 19, CPL 47 na PC 38. Sherehe hiyo
ilifanyika katika Chuo cha Polisi jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam nchini Tanzania, Suleiman Kova akitilia msisitizo jambo.
Askari wakiwa katika gwaride.
Coplo
Regina Mathias akipewa mkono wa pongezi na Kamanda wa Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam nchini Tanzania, Suleiman Kova, wakati wa sherehe ya
kuwazawadia vyeti vya sifa na zawadi kwa polisi wa Kanda Maalum ya Dar
es Salaam. Wanaoshuhudia ni polisi wenzake.
Askari Zuhura akipokea cheti kwa niaba ya wenzake.
Kila mmoja alionyesha ukakamavu.
Tukio
lililofurahisha ni pale wadau wa usalama barabarani walipojitokea
kumpongeza Askari wa Usalama Barabarani Mosses Senyagwa aliyekabidhiwa
zawadi ya pesa taslimu shilingi mil. 2.6 ikiwa ni zawadi ya utendaji
wake bora. Clouds Fm walitoa 500,000/=, Wadau/Vodacom 1,600,000/=, Big
Bon 300,000/= na Jeshi la Polisi 200,000/=. Zawadi hiyo alipewa askari
huyo kutokana ubunifu wake wa uongozaji wa magari.
Mtangazaji wa Clouds Fm Saidi Mohamed a.k.a Bonge akielezea jinsi mchakato ulivyoendeshwa wa kumpaka mshindi wa zawadi hiyo.
Bwana Albert Maneno ambaye ni mfanyakazi wa Vodacom Tanzania akiwa ameshika pesa zilizochangwa na wafanyakazi wenzake na wadau.
Bwana
Albert Maneno akimkabidhi pesa hizo Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam nchini Tanzania, Suleiman Kova ili aweze kumkabidhi Askari Mosses
Senyagwa.
Kamanda
wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam nchini Tanzania, Suleiman Kova
akimkabidhi kitita cha shilingi mil. 2.6 kwa Askari wa Usalama
Barabarani Mosses Senyagwa ikiwa ni zawadi kwa utendaji kazi wake bora.
Mwakilishi wa Big Bon akieleza zawadi waliyotoa wao.
Wakiwa katika picha ya pamoja.
Inspekta Solomoni Mwangamilo akikabidhiwa cheti na pesa taslimu laki mbili.
Wapo waliweza kujipatia zawadi za baskeli pamoja na pesa taslimu.
Kamanda Kova akitoa ripoti.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadiki akikagua siraha zilizokamatwa katika matukio mbali mbali ya uharifu.
Piki piki zilizotumika katika uharifu.
Mbwa wa Polisi akionyesha jinsi ya kukamata muarifu.
Askari wa Mbwa wakipita nao kwa ukakamavu.
Post a Comment