Picha ya kirusi cha Pithovirus sibericum kilichozinduka
Taarifa
ya kirusi aina ya Pithovirus sibericum ambacho kimekuwa bwete kwa miaka
zaidi ya 30,000 hadi kilipopelekwa tena kwenye mabara nchini Ufaransa
imeendelea kuwa taarifa kuu.
Kirusi hicho cha kale kimerejesha uhai wake baada ya kukaa bwete kwa miaka zaidi ya elfu 30,000 , walieleza wanasayansi .
Kilipatikana
kikiwa kimezama kwenye utando wa barafu katika eneo la Siberia, lakini
baada ya kuzinduliwa kikawa tena na uwezo wa kusababisha maambukizi .
Wanasayansi
wa Ufaransa wanasema hata hivyo kirusi hicho si hatari kwa maisha ya
binadamu na wanyama , lakini hii inaonyesha kuwa virusi wengine wanaweza
kuzinduka hata baada ya kuwa bwete kwa muda mrefu.
Taarifa ya utafiti huo ilichapishwa katika kituo cha kitaifa cha sayansi nchini Ufaransa (PNAS).
Professor
Jean-Michel Claverie, wa kituo cha utafiti (CNRS) katika chuo kikuu cha
Aix-Marseille nchini France, alisema: " Hii ni mara ya kwanza tumeona
kirusi ambacho bado kina maambukizi baada ya kipindi kirefu kama hiki.
Kirusi
hiki ambacho ni kikubwa kinaweza kuonekana kwa macho tofauti na virusi
vingine vinavyoonekana tu kwa kutumia microscope, na kilipatikana kikiwa
kimezikwa mita 30 chini kwenye barafu iliyoganda.
Wanasayansi
wanasema kubainika kwa kirusi cha Pithovirus sibericum kunaonyesha
hatari kwamba virusi vya maambukizi vinavyodhaniwa kuwa vimekufa
vinaweza kuibuka tena baada ya miaka mingi na kusababisha maambukizi
kutokana na shughuli za binadamu.Chanzo BBC Swahili


Post a Comment