Waziri
wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar Mh. Said Ali Mbarouk anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
tamasha la muziki wa kizazi kipya na tenzi, linalotajiwa kufanyika
katika viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es salaam kesho.
Tamasha hilo ni maalum kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar . Kauli mbiu za maadhimisho ya mwaka huu ni Utanzania wetu ni Muungano wetu tuulinde , tuuimarishe na kuudumisha.
Tamasha
hilo ni sehemu ya shughuli mbalimbali zinazotarajiwa kufanyika kuelekea
kilele cha Miaka 50 ya Muungano tarehe 26.4.2014.
Maadhimisho
ya miaka 50 ya Muungano yataambatana na shughuli mbalimbali
zitakazowashirikisha wananchi kupitia makangomano, michezo na burudani
na kilele chake itakua tarehe 26 Aprili,2014.
Shughuli
zitakazofanyika ni pamoja na kongamano na utengamano wa kikanda wa
Afrika Mashariki, kongamano la Bara la Afrika ,tamasha la muziki wa
dansi na taarabu , maonyesho ya Idara na Wizara za Muungano na mkesha
utakaofanyika kuamkia siku ya Muungano.
Aidha
maadhimisho haya ya miaka 50 ya Muungano yalizinduliwa Machi 1, 2014 na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein kwenye ukumbi wa Salama katika hoteli ya Bwawani Mjini Unguja
msisitizo ukiwekwa kwa wananchi kuendelea kudumisha udugu, amani, umoja na mshikamano.
Post a Comment