- Baada ya kushi nje kwa miaka takribani 30, nilirudi bongo moja kwa moja Miaka miwili na nusu iliyopita nikiwa nje nilikuwa kila siku ninaambiwa na kusoma kwamba Tanzania imebadilika sasa imekuwa tofauti na ile ya Baba wa Taifa na Rais Mwinyi niliyoiacha. Baada ya kurudi nimeamini kweli kwamba hii sio ile Tanzania tena ila ni nyingine kabisa, alama ya kwanza kuiona kwa macho yangu ilikuwa siku moja pale Uwanja wa Taifa kulikuwa na pambano la ngumi baina ya Wacheza Bongo Muvi Super Star Wolper na Wema Sepetu, nikakuta Uwanja wa Taifa umejaa full wananchi wanasubiri ngumi hizo, it was a shock to my bones mara yangu ya mwisho binafsi nilishirki kuujaza Uwanja Taifa na Halaiki ndio kitu pekee kilichoweza kuujaza uwanja kuacha mpiara wa Yanga na Simba enzi hizo.
- Jamani tuache kulalamika sana na yanayoendelea Dodoma sasa hivi kwenye Bunge la katiba, wale wabunge wanaofanya madudu kule ni sisi wenyewe wala tusilie sana, ndio Taifa tulilonalo sasa zile enzi za kina Mzee Kaduma, Mapunda Gisley, Eli Anangisye, Mwabulambo, Elinawinga, Dr. Kleruu, na the likes tayari zimepita kinachoendelea Dodoma sasa hivi ndio reality ya who we are now as a nation sasa lets work with what we have kuliko kulia lia on something we are not, wabunge wetu Dodoma hawakutoka mbinguni na tuache unafiki wa kujifanya kwamba sisi huku nyuma tukipewa zile nafasi tutafanya tofauti ni uongo wa mchana sana, tukubali tu kwamba wale wabunge ndio reality ya who we are now.
- Tukishakubali hiyo FACT then tutaweza kusonga mbele kuliko kulilia lilia what we are not, ukweli ni kwamba zile enzi za maadili hazipo tena sasa kila mtu na lwake, it is our new generation ya dotcom, electronics devices, fame, behind all these ndio unapata the character unayoiona Dodoma sasa hivi, inasikitisha sana lakini it is what it is na tuendelee kumuomba Mungu kwamba through this confused generation kutotaokea a great generation kwa sababu sometimes hasi na hasi huishia ku-create CHANYA!! yaani NEGATIVE + NEGATIVE = POSITIVE!!
Loading...
Home » Unlabelled » LE MUTUZ LIVE STRAIGHT TALK AT JAMIIFORUMS:- The Sad Truth is: Bunge la Katiba Dodoma Ni Reflection ya Taifa Letu la Sasa!
1 comments:
Belated thumb-up!
ReplyPost a Comment