Ni
habari ambayo inasisimua na kusikitisha kila ninapojaribu kukumbuka na
kugundua ni kwenye maisha halisi imetokea huku ikiwa imeondoka na abiria
239 ndani yake.Unaweza kujaribu kufikiria uone jinsi hili jambo lilivyo
zito.. ndege ya abiria imepotea kwa zaidi ya siku 11? sio kwamba
imepata ajali.. yani imepotea na haijulikani ilipo kwa zaidi ya siku 11?
msako umefanyika kwenye nchi zote ambazo labda ingekua huko kwa huo
muda lakini hakija onekana kitu.Taarifa iliyotoka kwa Wavuvi wawili
waliohojiwa March 19 2014, inasema wawili hawa ambao wakati huo walikua
baharini wamethibitisha kuiona ndege kubwa ya abiria ikipita chini sawa
na urefu wa miti.
Hiyo
iliwatisha mpaka kwenda kuripoti polisi ambapo muda mfupi baadae ndio
waliambiwa kuna ndege ya Malaysia imepotea na ilikua na abiria kuelekea
Beijing.
Ndugu wa
abiria waliokuwemo ndani ya ndege wameonekana kukata tamaa ya kusubiria
ndugu zao sasa hivi, mama mmoja mwenye ndugu kwenye ndege hii, Jumatano
ya March 19 2014 alibebwa baada ya kulilia ndugu yake kwa sauti kwenye
mkutano na Waandishi wa habari.
Taarifa
kuhusu hii ndege ni nyingi, ni siku moja tu imepita toka nisikie kwamba
muda mfupi baada ya ndege kupaa kutokea Malaysia, kuna mtu alizima kifaa
kinachohusika na mawasiliano na kuonyesha mwelekeo pamoja na speed ya
ndege.
Hii
hapa juu ni ndege ya jeshi ya Vietnam ikiwa kwenye msako wa ndege ya
Malaysia iliyopotea na kutoonekana kwenye radar na vyombo vingine
vilivyohusika kwenye msako wa ardhini na kwenye maji.
NA MILLAD
Post a Comment