“‘Short time’ vipi? Ni Sh.10,000 tu, gharama ya chumba kwangu.”
Hivi ndivyo nilivyopokelewa na binti wa miaka 21 katika Mtaa wa Uhindini
mkoani Dodoma nilikokwenda saa 4 usiku kufuatilia taarifa za kinadada
wanaofanya biashara haramu ya ngono, maarufu kama changudoa.
Uhindini ni mtaa maarufu mkoani Dodoma kwa
biashara ya ngono, ikifuatiwa na maeneo mengine kama Chako ni Chako,
Mwanga Bar na zaidi, katika kumbi za starehe kama Club 84 na Maisha.
Wakati nazungumza na binti huyo mfupi na maji ya
kunde, kinadada wengine kadhaa, walikuwa wakitufuatilia kwa karibu kuona
kama tumekubaliana au tumeshindwana bei ili na wao wataje gharama zao.
“Sh.8,000 huduma ya chapchap (short time)
chumbani, Sh.5000 hapa hapa na Sh.70,000 saa 5:00 (usiku) mpaka
asubuhi,” walijinadi wengine wakijaribu kile wanachokiita bahati yao.
Hata hivyo, baada ya kugundua kuwa sikuwa na lengo
la kufanya nao biashara, wote walirudi nyuma kusubiri wateja wengine.
Ndipo nilipomwita binti huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Monica
na kufanya naye mazungumzo kama ifuatavyo;
Mwananchi: Habari yako binti? Mimi niko hapa
kikazi na ningeomba nichukue dakika zako kadhaa ambazo nitazilipia kwa
Sh.10,000. Nilitamani kujua kazi hiyo ulianza lini na nini kilikusukuma
kuifanya?
Monica: Ni hadithi ndefu. Nilianza kuifanya mwaka
juzi nikiwa na umri wa miaka 19. Nililazimika kuifanya baada ya baba
yangu wa kambo kuonyesha kutokunijali kabisa na nikahisi sina thamani
kwenye familia yake.
Mwananchi: Wewe ni mwenyeji wa wapi na wateja wako ni kina nani hasa?
Monica: Mimi ni mtu wa Singida, naifanya biashara
hiyo sanasana hapa Dodoma wakati wa Bunge. Baada ya hapo narudi
kuendelea nayo huko huko Singida.
Mwananchi: Unatumia vigezo gani kupanga gharama za huduma zako?
Monica: Inategemea nazungumza na mtu mwenye
mwonekano gani. Gharama ya short time kwa mtu wa hali ya juu inaanzia
Sh.20,000 na kulala ni Sh.100,000 hapa malipo ya chumba kwangu. Kwa mtu
wa kawaida naanzia Sh.5000 short time hadi Sh.20,000 hii hakuna kulala.
Mama mtu mzima anayekadiriwa kuwa na kati ya umri
wa miaka 40 na 50 ambaye hakutaka kutaja jina lake, anaeleza kuwa
biashara ya ngono imemsaidia katika mambo mengi, ikiwamo kuwasomesha
watoto wake wawili; mmoja chuo kikuu na mwingine kidato cha nne.
Post a Comment