Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama
Salma Kikwete akizindua rasmi upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi
wakati wa kilele cha siku ya wanawake duniani katika sherehe
iliyofanyika katika uwanja wa Nyamagana huko Mwanza
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa
saratani ya mlango wa kizazi aliwakabidhi Waganga wakuu wa mikoa ya
Mwanza, Iringa, Mbeya na Mara vifaa vya kupima saratani hiyo. Pichani
Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.
Valentino Bangi mkoba wenye vifaa vya upimaji.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Nestory
Masalu kutoka hospitali ya Rufaa ya Bugando ambaye alikuwa akiwapima
akina mama katika kituo cha Afya cha Buzuruga kilichoko katika wilaya ya
Ilemela mkoani Mwanza mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa saratani
ya mlango wa kizazi katika uwanja wa Nyamagana na kutembelea kituo
hicho ambapo wanawake wengi walijitokeza kwa ajili ya kupima.
Post a Comment