Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA BUNGE LA KATIBA MJINI DODOMA LEO


Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Pandu Ameir Kificho akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba alipowasili katika ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma kushoto kwake ni Bw. Mohamed Mbwana, katikati ni Rufai said Rufai na Kulia kwa Mwenyekiti ni Bw. Heri Khatibu.
Mjumbe wa Bunge la Katiba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Hawa Ghasia na Naibu Waziri Wizara ya Uchukuzi Charles Tizeba wakiwasili katika ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge la Katiba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Hawa Ghasia akitoa mapendekezo juu ya taratibu za kupiga kura katika kufanya marekesho ya kanuni zitakazotumika katika Bunge Maalum la Katiba, wakati wa Semina ya Kujadili kanuni zaitakazoongoza Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akiwaeleza jambo Waziri wa Fedha Saada Salum Mkuya (katikati) na Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi(Kushoto). Wakati wa Semina ya Kujadili kanuni zaitakazoongoza Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba akitoa mapendekezo yake kuhusu taratibu za upigaji kura unaoangalia maridhiano ya misingi ya kidemokrasia .Kulia ni Waziri Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi Maalum Prof. Mark Mwandosya na mbele ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa.wakati wa Semina ya Kujadili kanuni zaitakazoongoza Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.
 
(PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO)
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top