STRAIKA
Mahiri wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta, Leo huko Lubumbashi amibeba
Timu yake TP Mazembe ilipoifunga Sewe Sports ya Ivory Coast Bao 1-0 kwa
kufunga Bao hilo pekee katika Dakika ya 66 na kuiingiza hatua ya Makundi
ya CAF CHAMPIONZ LIGI.
Katika Mechi ya Kwanza Wiki iliyopita
huko Ivory Coast, TP Mazembe walifungwa Bao 2-1 na Matokeo ya Leo
yamefanya Jumla ya Magoli kuwa 2-2 na Mazembe kupita kwa Bao la Ugenini.
Katika Mechi hii ya Leo, TP Maze,be walikosa Penati iliyopigwa na Jonas Sakuwaha kwenye Dakika ya 53.
Droo ya kupanga Makundi mawili ya CAF
CHAMPIONZ LIGI itafanyika hapo Jumanne Aprili 29 kwenye Makao Makuu ya
CAF Jijini Cairo Nchini Misri.
CAF CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
Marudiano
Jumamosi Machi 29
TP Mazembe - Congo, DR 1 Sewe Sport - Ivory Coast 0 [Matokeo Mechi mbili 2-2, TP Mazembe yasonga kwa Bao la Ugenini]
Al Ahly – Egypt v Al Ahli - Benghazi – Libya [0-1]
Kaizer Chiefs - South Africa v AS Vita Club - Congo, DR [0-3]
Club Sportif Sfaxien – Tunisia v Horoya Athlétique Club – Guinea [1-0]
Jumapili Machi 30
Al Zamalek – Egypt v Nkana FC – Zambia [0-0]
Coton Sport FC – Cameroon v Entente Sportive de Sétif – Algeria [0-1]
Espérance Sportive de Tunis – Tunisia v AS Real de Bamako – Mali [1-1]
Al-Hilal – Sudan v AC Leopards de Dolisie – Congo [1-1]
**Ratiba inaweza kuwa na Mabadiliko
++++++++++++++++++++++++++++++++
DONDOO MUHIMU:
-DROO YA KUPANGA MAKUNDI Tarehe 29 Aprili 2014
-MAKUNDI YATAKUWA MAWILI YA TIMU 4 KILA MOJA NA KUCHEZA MTINDO WA LIGI, NYUMBANI NA UGENINI
-WASHINDI WAWILI WA JUU WA KILA KUNDI WATAINGIA NUSU FAINALI
++++++++++++++++++++++++++++++++
CAF KOMBE LA SHIRIKISHO
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
Machi 29
ZESCO United FC – Zambia v Medeama – Ghana [0-2]
Difaa Hassani El Jadidi – Morocco v AS Kigali – Rwanda [0-1]
Bayelsa United – Morocco v How Mine – Zimbabwe [1-2]
Supersport United - South Africa v E.S. Sahel – Tunisia [0-1]
Machi 30
Djoliba AC – Mali v Wady Degla – Egypt [0-2]
Petro Atlético de Luanda – Angola v Al Ismaily – Egypt [0-0]
Supersport United - South Africa v E.S. Sahel – Tunisia [0-1]
C. A. Bizertin – Tunisia v Warri Wolves – Nigeria [0-0]
ASEC Mimosas Abidjan - Ivory Coast v CS Constantine – Algeria [0-1]
**Ratiba inaweza kuwa na Mabadiliko
soka In Bongo
Post a Comment