Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Meli ya Korea Kaskazini yanaswa Libya




Meli ya mafuta nchini Libya
Wakuu nchini Libya, wamesema kuwa wameikamata meli moja iliyokuwa na bendera ya Korea Kaskazini, ikiwa na shehena haramu ya mafuta katika bandari inayodhibitiwa na waasi.
Msemaji wa shirika la kitaifa la mafuta, amesema kuwa meli hiyo ilisimamishwa ilipokuwa ikijaribu kungoa nanga na kwa sasa inasindikizwa katika bandari inayodhibitiwa na serikali ya Libya.
Maafisa wa serikali ya Libya waliisimamisha Meli hiyo ya Korea Kaskazini ilipokuwa ikiondoka kutoka bandari inayodhibitiwa na waasi siku ya Jumatatu ikiwa imesheheni mzigo usio rasmi wa mafuta ghafi.
Jeshi la nchi hiyo limethibitisha tukio hilo.
Waasi wa zamani wanaotaka kuitenga eneo la Libya Mashariki, wamekuwa wakimiliki bandari ya Al-Sidra na vituo vingine muhimu vya kuuzia bidhaa nje katika eneo hilo tangu Julai mwaka uliopita.
Mnamo siku ya Jumamosi, walianza kupakia shehena ya mafuta yasiyosafishwa ndani ya meli hiyo ya Korea Kaskazini iitwayo Morning Glory, iliyokuwa imetia nanga katika bandari ya Al-Sidra.

Viongozi walaani wizi wa mafuta

Kiwanda cha mafuta nchini Libya
Siku ya Jumatatu jeshi la wanamaji lilizuilia meli hiyo ilipokuwa ikiondoka bandarini, huku amri ikitolewa ielekezwe hadi katika bandari inayodhibitiwa na serikali.
Chama kikuu cha kisiasa nchini humo cha General National Congress, GNC, kimethibitisha kuzuiliwa kwa meli hiyo.
Runinga ya taifa Nchini Libya Al-Nabaa pia imeripoti tukio hilo kwa undani.
Walid al-Tarhuni, ambaye ni msemaji wa zamani wa kundi la waasi ambalo limekuwa likidhibiti bandari hiyo, ameiambia runinga ya Al-Nabaa kuwa meli hiyo ya mizigo ilikuwa ikielekea katika bandari ya Zawiyah, kilomita 50, Magharibi mwa mji mkuu Tripoli, kupakua mafuta hayo.

Utawala wa Washington umesema kuwa umeshangazwa na tukio hilo na kukariri kuwa mafuta inayotoka Libya ni mali ya raia wa nchi hiyo na wala sio ya makundi fulani.Chanzo BBC Swahili
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top