Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MESUT OZIL NJE MWEZI MMOJA!!

 

Mesut Ozil atakuwa nje ya Uwanja kwa muda usiopungua Wiki 4 baada uchunguzi wa kina kuthibitisha kuumia kwake kwa Musuli za Pajani (Hamstring).
Kiungo huyo wa Arsenal mwenye Miaka 25 aliumia katika Dakika ya Pili tu ya Mechi ya Jumanne Usiku ya UEFA CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Bayern Munich ambayo walitoka Sare 1-1 na kutolewa nje ya Mashindano hayo lakini alijikongoja kucheza hadi Haftaimu alipobadilishwa.
Ozil, ambae alisainiwa kwa Dau la Rekodi kwa Arsenal ya Pauni Milioni 42.4 kutoka Real Madrid mwanzoni mwa Msimu huu, ataikosa tripu ya Arsenal kwenda huko White Hart Lane Jumapili hii kucheza Dabi ya London ya Kaskazini dhidi ya Mahasimu wao Tottenham kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Pia Ozil atazikosa Mechi na Chelsea, Swansea, Manchester City na Everton.
Hizo zote ni Mechi muhimu za Ligi Kuu England ambazo Arsenal ipo mbioni kupigania Ubingwa.
Mbali ya Mechi hizo, Ozil pia ni hatihati kuikosa Mechi ya Nusu Fainali ya FA CUP dhidi ya Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo, Wigan Athletic, hapo Aprili 12 Uwanjani Wembley.
Tangu ajiunge na Arsenal, Ozil amefunga Bao 6 katika Mechi 35.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top