Mwanamume mmoja aliyeishi jela kwa zaidi ya miaka 25
akisubiri hukumu ya kifo nchini Marekani, ameachiliwa huru baada ya
mahakama kubatilisha uamuzi wa mahakama kuwa alikuwa na hatia ya mauaji
yaliyotokea mwaka 1983.
Glenn Ford, 64, alikuwa jela akisubiri hukumu ya kunyongwa tangu mwaka 1988 mwezi Agosti.
Mahakama wakati huo ilimpata na
hatia ya mauaji ya Isadore Rozeman aliyekuwa na umri wa miaka 56 akiuza
mikufu. Bwana Ford alikuwa mfanyakazi wake wakati huo.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa ni mmoja wa wafungwa waliohukumiwa kifo kwa muda mrefu nchini humo na kuachiliwa.
Glenn alisema kuwa anahisi vizuri sana kwamba ameachiliwa.
Alisema ana maudhi ndani ya moyo wake kutokana
na kufungwa bila hatia kwa kitu ambacho hakukifanya na kuwa amepoteza
muda wake mwingi jela.
"miaka 30 ya maisha yangu. Siwezi kufanya mambo
ambayo ningefanya nikiwa na umri wa miaka 35, 38 au 40. Mwanangu
nilipofungwa jela alikuwa mtoto sasa ni mtu mzima na watoto wake.''
Jaji aliymwachilia huru bwana Ford, Ramona
Emanuel alisema Jumatatu kuwa kulikuwa na ushahidi mpya kuonyesha kwamba
Bwana Ford, hakuhusika na mauaji hayo.
Makosa mengi yalipatikana katika kesi dhidi ya Ford kama yalivyoelezwa na vyombo vya habari nchini Marekani.
Inaarifiwa kuwa kesi ya Ford iliendeshwa na mawakili ambao hawakua na ujuzi wa kazi.
BBC
Post a Comment