Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MKE AUWAWA NA MUMEWE KWA KUGOMA KUFANYA MAPENZI KITANDA KIMOJA NA MKE MWENZIE HUKO GEITA...!!


 


Mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina la Constancia John (28) Mkazi wa kijiji cha Ichwankima wilayani Chato mkoani Geita,  amefariki dunia baada ya kupigwa na mume wake Joseph Clemence(34) kwa tuhuma ya kumnyima tendo la ndoa.
 
Tukio hilo limetokea majira ya saa sita usiku wa kuamkia jana baada ya Clemence kumpiga mkewe Constancia na kumburuza kutoka nje hadi kumuingiza ndani, na baadae ya kufariki dunia kutokana na kipigo hicho.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema chanzo cha mgogoro huo ni Clemence ambaye  ana wake wawili kuwalazimisha kulala nao chumba kimoja kwa ajili ya tendo la ndoa, jambo ambalo Constancia alilikataa na kusababisha ugomvi huo
 
Kamanda wa polisi mkoani Geita kamishina msaidizi mwandamizi Leonard Paul  amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Tukio hili linakuja ikiwa ni siku chache tu baada ya kuazimisha siku ya wanawake duniani, huku mojawapo ya  agenda kuu ya maazimisho hayo ikiwa ni kupinga ukatili na udhalilishaji dhidi ya wanawake.

Kufuatia tukio hilo katibu wa kituo cha sheria na haki za binadamu wilayani Geita Elineema Charles ametaka hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi ya Clemence, na kuwa fundisho kwa wengine kwani kitendo hicho hakivumiliki katika jamii.

Na valence Robert
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top