MKURUGENZI
wa Mashitaka Nchini (DPP), amemfutia mashitaka aliyekuwa Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime (61) na kisha kumuunganisha na wenzake
11 na kuwasomea upya mashtaka 27 ya mauji katika mtaa wa Indira Gandh,
yaliyotokana na kuporomoka jengo la ghorofa 16.
Mbali
na Fuime washtakiwa wengine ni, Diwani wa Kata ya Goba, Ibrahim Mohamed
maarufu kama Kisoki, Raza Ladha, Goodluck Mbanga, Willbroad
Mugyabuso,Mohamed Abdulkarim, Charles Ogare, Zonazea Oushoudada, Vedasto
Ruhale, Michael Hema, Albert Mnuo na Joseph Ringo.
Washtakiwa
hao walisomewa hati mpya ya mashitaka baada ya kuondolewa hati ya
zamani ya mauaji ya bila kukusudiwa na kuunganishwa Fuime na idadi yao
kufikia 12, mbele ya Hakimu Mkazi Devota Kisoka.
Upande
wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Benard Kongola
akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka na Wakili wa
Serikali Joseph Maugo.
Kongola
alidai kuwa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha 294 kidogo cha (1) upande
wa Jamhuri unaomba ridhaa ya mahakama ya kumuongeza mshtakiwa Fuime
katika hati mpya ya mshitaka.
Hakimu Kisoka alisema mahakama haina pingamizi na maombi ya Jamhuri ya kubadilisha hati ya mashitaka dhidi ya washtakiwa.
Jamhuri
ilidai kuwa katika shtaka la kwanza, Machi 29, mwaka 2013 mtaa wa
Indira Gandh, Wilaya ya Ilala washtakiwa kwa pamoja walimuua kwa
makusudi Yusuph Khari.
Alidai katika shtaka la pili na la tatu, Machi 29, mwaka 2013 washtakiwa waliwaua kwa makusudi Kulwa Alfani na Hamada Musa.
Katika
shtaka la nne na la tano, ilidaiwa kuwa Machi 29, mwaka 2013 katika
mtaa huo, washtakiwa wote kwa pamoja waliwaua kwa makusudi Kessy Manjapa
na Khamis Mkomwa.
Kongola
alidai katika shtaka la sita na la saba, Machi 29, mwaka 2013 katika
mtaa huo, washtakiwa waliwaua kwa makusudi Boniface Bernad na Suhail
Karim.
Upande
huo wa Jamhuri ulidai katika shtaka la nane na la tisa, Machi 29, mwaka
2013 katika mtaa huo, washtakiwa wote kwa pamoja waliwaua kwa makusudi
Salmani Akbar na Selemani Haji.
Wakili
wa serikali Maugo aliendelea kusoma hati hiyo ya mashtaka alidai
katika shtaka la 10 na 11, Machi 29, mwaka 2013 katika mtaa huo,
washtakiwa wote kwa pamoja waliwaua kwa makusudi Selemani Mtego na
Sikudhani Mohamed.
Ilidaiwa
katika shtaka la 12 na 13, Machi 29, mwaka 2013 katika mtaa huo,
washtakiwa wote kwa pamoja waliwaua kwa makusudi Ahmed Milambo na Salum
Mapunda.
Shtaka
la 14 na 15, ilidaiwa kuwa Machi 29, mwaka 2013 katika mtaa huo,
washtakiwa wote kwa pamoja waliwaua kwa makusudi Suleimani Mnyani na
John Majewa.
Shtaka
la 16 na 17, ilidaiwa kuwa Machi 29, mwaka 2013 katika mtaa huo,
washtakiwa wote kwa pamoja waliwaua kwa makusudi Mussa Mnyamani na
David Herman.
Kweka
alidai katika shtaka la 18 na la 19 kwamba Machi 29, mwaka 2013 katika
mtaa huo washtakiwa waliwaua kwa makusudi William Joakim na Abdulrahman
Mwiha.
Alidai
katika shtaka la 20 na 21 kwamba Machi 29, mwaka 2013 mtaa wa huo,
washtakiwa wote kwa pamoja waliwaua kwa makusudi Jumanne Athuman
na Advai Mpinge.
Wakili
huyo aliendelea kusoma hati hiyo, shtaka la 22 na la 23, alidai kuwa
Machi 29, mwaka 2013 mtaa huo washtakiwa wote kwa mapoja waliwaua kwa
makusudi Emmanuel Wahai na Agustino Chuma.
Katika
shitaka la 24 na 25, ilidai kuwa Machi 29, mwaka 2013 katika mtaa huo,
washtakiwa wote kwa pamoja waliwaua kwa makusudi Phillipo Kusimala na
Said Abbas.
Maugo
aliendelea kudai katika shitaka la 26 na 27, Machi 29, mwaka 2013 katika
mtaa huo, washtakiwa wote kwa pamoja waliwaua kwa makusudi Bethod
Mwanengule na Gabriel Kamwela .
Kwa
mujibu wa Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA), mashitaka
yanayowakabili washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote hadi pale upelelezi
wa kesi hiyo utakapokamilika itahamishiwa Mahakama Kuu Tanzania, Kanda
ya Dar es Salaam kwa ajili ya kusikilizwa.
Hakimu Kisoka alisema kesi hiyo itatajwa Machi 26, mwaka huu na washtakiwa dhamana yao imefutwa wapelekwe mahabusu.
Jana
saa 3:00 asubuhi upande wa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Augustino
Mmbando uliwasilisha hati ya Nole kutoka kwa DPP ikieleza kwamba hana
nia ya kuendelea kumshitakiwa Fuime na kuomba kumfutia mashtaka hayo.
Hakimu
Mmbando alifuta mashitaka hayo, lakini askari kanzu wa jeshi la Polisi
walimuweka chini ya ulinzi na baadaye alipandishwa kizimbani mbele ya
Hakimu Kisoka na kuunganishwa na wenzake.
Post a Comment