Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MKUU WA WILAYA AZITAKA KAMPUNI ZA HISA KUJIWEKEA UTARATIBU WA KUWAELIMISHA WATANZANIA JUU YA UMUHIMU WA MASOKO YA HISA

indexNa Gladness Mushi, Arusha
Mkuu wa  wilaya ya Arusha John Mongela ametoa wito kwa makampuni ya hisa hapa nchini kuhakikisha kuwa yanajiwekea utaratibu wa kutoa elimu kwa watanzania juu ya umuhimu wa kuweka na kununua hisa kwani takwimu bado zinaonesha kuwa asilimia kuwa ya watanzania bado uelewa wao upo chini sana.

Mongela aliaysema hayo wakati akiongea na wajasiriamali pamoja na wadau wa mfuko wa soko la hisa la Dar es saalam DSE mapema jana jijini Arusha.
Alibainisha kuwa kwa sasa masoko ya hisa ni mengi sana lakini asilimia kubwa ya watanzania bado hawajaweza kuwa na uelewa wa kutosha juu ya umuhimu wake hali ambayo inatakuiwa itatuliwe tena kwa haraka sana.

Katika hatua nyingine Mongela alidkuwa ili uchumi wa nchi ya Tanzania uweze kukua  ni lazima hata wajasirimali nao waweze kubebwa kwa kupewa elimu sanjari na mbinu za kuwafikisha katika malengo yao mbalimbali.

“kama tukiwawekea utaratibu mzuri hawa wajasiriamali lakini pia
wafanyabiashara wadogo basi mitaji itaongezeka na wataweza kujiendesha
wao wenyewe na hivyo uchumi wa nchi nao utaweza kuimarika kwani uwezo
huo upo kabisa”aliongeza Mongela.
Naye Mwanasheria wa soko hilo la hisa la Dar es saalam. Mary Muniwasa
alisema kuwa kwa kutambua  umuhimu wa wafanyabishara wadogo na wa
daraja la kati wameanzisha rasmi dirisha la kukuza ujasiriamali kwa
malengo ya kuboresha uchumi wa nchi.
aliwataka wafanya biashara wote hapa nchini kuhakikisha kuwa wanatumia
vema dirisha hilo la kukuza ujasiriamali kwa maslahi ya kuboresha
uchumi na maendeleo ya Nchi ya Tanzania.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top