Mtoto Said Siraji akiwa amelazwa hospitalini baada ya kukatwa shingo na Baba yake
Mtoto
Said Siraji(13), mkazi Majengo Kaskazini wilayani Kahama mkoani
Shinyanga aliyedaiwa kukakatwa shingo na baba yake usiku wa kuamkia
Machi nne mwaka huu, amefariki dunia leo mchana katika Hospitali ya
Rufaa ya Bugando mjini Mwanza.
Mwenyekiti
wa Kitongoji cha Majengo Kaskazin Noel Makula Mseven amesema Marehemu
Siraji aliyekuwa anasoma darasa la tatu katika Shule ya Msingiya Majengo
amefariki akiwa Bugando alikokuwa amelazwa kwa matibabu zaidi mara
baada ya hali yake kuwa mbaya katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
Kwa
mujibu wa mama mzazi wa Siraji Mariamu Idd awali alieleza, siku ya tukio
Marehemu Siraji alichukuliwa na baba yake mzazi anayeitwa Siraji
Salvatory(45) kwenda naye kwake mitaa ya Majengo kwa kuwa wazazi hao
walikwishaachana siku nyingi
Alfajiri
ya Machi nne Salvatory ambaye kwa sasa yuko Rumande alimchukua Siraji na
kumpeleka kwenye makaburi ya majengo kwa nia ya kumchinja lakini
hakufanikiwa kumuua huku akimwachia jeraha likimwaga damu nyingi kabla
hajaokotwa na wasamaria na kupelekwa hospitalini.
Museven
amesema Julai mwaka jana Salvatory alitaka kumchinja mke wake Mariam
lakini akaokolewa na Mseven kitu kilichomuuzi salvatory na kutaka
kumchinja mwenyekiti huo wa kitongoji tuhuma iliyompeleka gerzani kwa
kipindi cha miaka miwili..
Hata
hivyo mseven amesema siku amemwokoa mariam Salvatory alitaka kumchinja
mtoto wa jirani ili kutimiza azma yake ikashidikana hali inayodhaniwa
sasa imekamilika baada ya kumchinja mtoto wake Marehem Siraj
Habari
ambazo hazijathibitishwa na idara ya upelelezi wilayani humo zimesema,
Salvatory amewaeleza maafisa wa polisi kwamba kitendo hicho amekifanya
kwa lengo la kulipa mchango wa Freemason na kwamba alitaka kuchangia
damu ya mtoto mdogo akakataliwa.
Mauaji
haya yametokea kwa wakati jamii ya wana kahama inakabiliwa na balaa la
kuamini vitu na mambo yasiyo na msingi kama lile la kubaini wachawi na
imani ya Freemason ambayo haijulikani hata ilikotoka wala msingi wake.
CHANZO : MDOSOAJI
CHANZO : MDOSOAJI
Post a Comment