Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MTUMBWI WAZAMA BAHARINI HUKO MTWARA, HABARI KAMILI IPO HAPA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVkEGlv5WK2580jmmpNXan7d4q2EeJOMGyYpaOAujdKY4veuV0-HgyIPXn6OyuCCV7dsXoii7xKL572x5yu3nituX4ATH8ww91j4sD45Ea7m5fVpoc-TFqh8ZugQvsgMMVyYZZlv__ZDQ_/s1600/DSC_0927.JPG

Taarifa kutoka Mtwara ambazo zimethibitishwa na jeshi la Polisi Mtwara ni kuhusu Mtumbwi ambao umezama wakati ukivuka kutoka kitongoji cha Ng’wale kwenda ng’ambo ya pili ambapo ndiyo sehemu waliyokuwa wanashukia abiria waliokuwepo lakini kabla hawajafika upande wa pili mtumbwi huo ulizama.
Tayari Watu 21 wamefikishwa katika hospital ya mkoa wa Mtwara kwa matibabu ambao wote ni wakina mama pamoja na mtoto mmoja wa kiume wa mwaka 1,waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo ni wakina mama 3
Mtumbwi huo unahisiwa ulikuwa na abiria 24 pamoja wahusika wa mtumbwi huo wawili kwa pamoja jumla ya watu waliokua kwenye mtumbwi huo ni 26,wakina mama hao walikua wanatoka kutafuta samaki kwa ajili ya biashara.
Jeshi la polisi bado linamtafuta Dereva wa Mtumbwi huo ambaye inasemekana aliogelea na kutoweka baada ya mtumbwi kuzama
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika ingawa baadhi ya abiria wanadai ni upepo mkali na mvua iliyokuwa inanyesha.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top