Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mwanafunzi wa Darasa la Pili aandika Kuhusu Yesu,Mwalimu amsihi abadili Mada

 


Kazi ya Ryleigh yenye kichwa cha habari "Yesu ni mshindi wangu"©WCET-TV.
Uongozi wa shule ya msingi ya Cerro Gordo Elementary iliyopo kaskazini mwa Carolina nchini Marekani imeripotiwa kumkataza mwanafunzi wa kike aitwaye Ryleigh Watts (8) kutoandika kuhusu Yesu katika kazi anazopewa kufanya shuleni, baada ya mwanafunzi huyo kuandika insha inayosema Yesu ni mshindi wake.

Kutokana na tukio hilo mama mzazi wa
mwanafunzi huyo aitwaye Heather Watts amesema binti yake anayesoma darasa la pili shuleni hapo aliambiwa na mwalimu wake kutafuta mada nyingine ya kuandika badala ya hiyo aliyoiandika ya kumuhusu Yesu, ambapo mama huyo anamtuhumu mwalimu kwakumuuliza mwanaye swali ambalo halikuwa vizuri "kwani huwezi kuandika kitu kingine?", ndivyo mwalimu huyo alivyouliza.

Mama Ryleigh amekiambia kituo cha runinga kiitwacho WCET-TV kwamba swali hilo halikuwa zuri, kwani kwa maoni yake anadhani ni vizuri watoto wakapewa uhuru wa kuandika chochote wanachojisikia, kama anataka kuandika kuhusu Yesu, aachiwe aandike kuhusu Yesu", amekaririwa mama huyo. Aidha kituo hicho cha runinga kimerusha sehemu ya kazi iliyoandikwa na mwanafunzi hiyo ikisema "Mshindi wangu ni Yesu, kwakuwa ananisaidia, na kunifanya mwema, pia anawezesha mambo mazuri kutendeka".

Heather amesema hajafurahia swali aliloulizwa mwanae kwakuwa si haki na kinamnyima mtoto uhuru wa kujieleza na uhuru wa dini. Kwa upande wa uongozi wa kata ya Columbus iliko shule hiyo umekana kutokea kwa jambo hilo wakisema kwamba baada ya kuongea na mwalimu pamoja na mkuu wa shule wanafunzi hawakushinikizwa katika kuchagua mada yeyote ya kuandika, uongozi wa kata hiyo unaruhusu wanafunzi kupewa uhuru wa kujieleza katika wigo wote wa elimu, pamoja sera za wazi. Aidha umewaomba wazazi na walezi kuwasiliana ama kuwatembelea watoto wao shuleni na kufikisha jambo lolote walilonalo.

Baada ya tambo hilo la kata, mama huyo amesema alikutana na mwalimu pamoja na mwalimu mkuu wa shule hiyo lakini tatizo hilo halijarekebishwa kwakuwa mtoto wake bado ameambiwa atafute mada nyingine ya kuandika na sio hiyo ya Yesu. Tukio hilo si la kwanza kuripotiwa, kwakuwa baadhi ya wanafunzi nchini humo wamekuwa na kawaida ya kuzungumzia masuala yao ya dini katika kazi zao za shule.

Chanzo : BC
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top