Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Mwishehe Mhalinze wakati wa mkutano wa
kampeni uliofanyika kijiji cha Kibindu na kuhudhuriwa na wakazi wa
kijiji hicho, akimuombea kura Ridhiwani Kikwete mgombea wa kupitia Chama
cha Mapinduzi amemfananisha mgombea huyo na Jeki aina ya (Tanganyika
Jack) na kusema atawakwamua wana Chalinze katika changamoto zinazowakabili
katika maendeleo jimboni humo,Uchaguzi mdogo wa jimbo la Chalinze
unatarajiwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu
Kada
wa Chama cha Mapinduzi kutoka UVCCM makao makuu Mtela Mwapamba
akizungumza na wanakibindu katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika
kata hiyo leo.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo wa kampeni
Msanii Puto akifanya vitu vyake katika mkutano huo.
Wananchi wa kijiji cha Pera kata ya Kibindu wakiserebuka kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni kijijini hapo.
Baadhi
ya wananchi wa kijiji cha Kwamkonje kata ya Kibindu wakifuatilia kwa
makini hotuba ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Mwishehe Mlau
hayupo pichani.
Baadhi
ya wananchi wa kijiji cha Kwamkonje kata ya Kibindu wakifuatilia kwa
makini hotuba ya Mtela Mwapamba kutoka UVCCM makao makuu. Changamoto za ubovu wa Barabara kutokana na mvua leo pia ziliukabili msafara huo.
Wakati mwingine ilibidi kuweka sawa barabara ili kuhakikisha msafara unapita na kuendelea na ratiba yake kama kawaida.
Magari yakipita kwa kasi ili kuhakikisha hayanasi katika matope hayo.
.(PICHA NA KUKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KIBINDU-CHALINZE)
Post a Comment