Mwanajeshi
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Muhsin Kombo
amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela baada ya kupatikana na hatia ya
kughushi.
Hakimu Mkazi Waliarwande Lema wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, alitoa hukumu hiyo jana baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi 19 na vielelezo vya upande wa Jamhuri pamoja na utetezi wa washitakiwa.
Hakimu Mkazi Waliarwande Lema wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, alitoa hukumu hiyo jana baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi 19 na vielelezo vya upande wa Jamhuri pamoja na utetezi wa washitakiwa.
Kombo na mkewe Devotha Soko walikuwa wanakabiliwa na mashitaka sita ya kupanga njama, kughushi, kutoa taarifa za uongo na kujipatia Sh milioni 100 kwa njia ya udanganyifu.
Katika hukumu yake jana, Hakimu Lema alimuachia huru Devotha kwa kuwa upande wa Jamhuri ulishindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yake na Kombo alitiwa hatiani kwa shitaka la kughushi.
Kombo ametiwa hatiani kwa mashitaka ya kughushi muhtasari wa kikao kilichofanyika Machi 25 mwaka 2008 akionesha kuwa, Devotha amechaguliwa na familia ya marehemu Awadh Ally kusimamia mirathi.
Katika mashitaka mengine ilidaiwa Mei 5 mwaka 2008 katika Mahakama ya Mwanzo Sinza, jijini Dar es Salaam, washitakiwa walitoa taarifa za uongo kwa Hakimu wa Mahakama.
Inadaiwa walitoa taarifa kwamba Ally alifariki mwaka 1986 na kuacha watoto wawili, jambo lililosababisha hakimu huyo kumteua Devotha kuwa msimamizi wa mirathi.
Aidha inadaiwa Januari 28 mwaka 2011, washitakiwa walijipatia Sh milioni 100 kutoka kwa Rukia Zidadu kwa madai ya kumuuzia nyumba yao iliyopo Kijitonyama katika kiwanja namba 281 block 46.
Post a Comment