Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

REAL YAUA 5-0 LA LIGA

Konde hilo: Gareth Bale akishangilia baada ya kuifungia Real katika ushindi wa 5-0Breakthrough: Cristiano Ronaldo celebrates after putting Real ahead on 14 minutes, his 28th La Liga goal of the season
Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Real bao lake la 28 katika msimu huu wa La Liga

*******
 
NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale walirejesha urafiki wao tena wakati timu yao ikiifumua mabao 5-0 Rayo Vallecano usiku huu katika mchezo wa La Liga uliofanyika Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Bale alimsetia Ronaldo kuifungia Real Madrid bao la kwanza dakika ya 14, na akachangia bao la pili lililofungwa na Carvajal dakika ya 54, kabla ya kufunga la tatu dakika ya 67 na la nne dakika ya 70 wakati Morata alifunga la tano dakika ya 77.
Real sasa inatimiza pointi 73 baada ya mechi 31, lakini inaendelea kuketi nafasi ya tatu nyuma ya Barcelona yenye pointi 75 na Atletico Madrid pointi 76 kileleni, zote zikiwa zimecheza mechi 31 pia.
Ronaldo alimkasirikia Bale baada ya kwenda kupiga mpira wa ovyo dakika za mwishoni Real ikilala 4-3 mbele ya Barcelona wiki iliyopita, lakini leo amemaliza hasira za mchezaji mwenzake huyo na kurudisha urafiki wao tena.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top