Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RIDHIWANI KIKWETE ADHAMIRIA KUWAKOMBOA WANA CHALINZE



Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi akimnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete kwa Wananchi wa Kijiji cha Kibindu,Kata ya Mbwewe,Bagamoyo leo Machi 16,2014.
 Wananchi wa Kijiji cha Kwaruhombo,Kata ya Mbwewe,Bagamoyo wakiwa wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa Kijiji hicho ili kuweza kumsikiliza Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete (hayupo pichani).
 Diwani wa Kata ya Mbwewe,Omari Mhando akisisitiza jambo kwa Wananchi wa Kijiji cha Kwamuhombo wakati wa Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete (hayupo pichani) uliofanyika leo Machi 16,2014 kwenye Uwanja wa Kijiji hicho.
 Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akipiga stori na vijana wa Kijiji cha Kwamduma.
 Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akifurahi jambo kwenye moja ya mikutano yake.Kulia ni Diwani wa Kata ya Kibindu,Mkufya Ramadhan.
Wazee wakifurahia moja ya Jambo lililo wagusa.
 Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akisalimiana na wanakijiji wa kijiji cha Kwamsanja,wakati alipofika kwa ajili ya kuzungumza nao na kuwaomba kura katika Uchaguzi huo.
 Wananchi wa Kijiji cha Kibindu wakiwa wamejitokeza kwa wingi Mkutanoni.
Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kibindu wakati akiwaomba kumpigia Kura Mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo,Ridhiwani Jakaya Kikwete .
Nyomi la kweli kweliiiii....
Popote walipo ni CCM Damu....


Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kwaruhombo,leo Machi 16,2014.Ridhiwani Kikwete ameahidi kuyashughulikia Matatizo mbali mbali wanayokabiliana nayo Wananchi wote wa Jimbo la Chalinze,yakiwemo ya Barabara,Maji,Elimu,Matibabu na mengine mengi ambapo amesema atayafanyia kazi atakapopewa ridhaa ya kuwa kiongozi wa Wanachalinze.
Mkutano ukiendela.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete wapungua mkono wananchi wa Kijiji cha Kwarihombo,wakati alipokuwa akiwasili kwenye Kijiji hicho,leo Machi 16,2014.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kulia) akimsikiliza kwa makini Mlemavu wa miguu,Hamis Ibrahim Mkazi wa Kijiji cha Kwarihombo,ambaye alikuwa akimuomba Mgombea huyo msaada wa kupatiwa Baiskeli ya kulembelea kutokana na kwamba aliyonayo imechoka sana.Ridhiwani ameahidi kumpelekea Baiskeli mpya ya kutembelea Mlemavu huyo.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akifurahi jambo na Mtoto aliejitambulisha kwa jina la Zungu,wakati apofika kuwasalimia wazee wa Kijiji cha Kwamduma.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwa ameungana na wananchi wa Kijiji cha Kwamduma,Kata ya Kibindu kwenye Msiba wa Mtoto wa Mzee Juma Mkonje (hayupo pichani) uliotokea leo Machi 16,2014.
Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi akizungumza wakati akitoa pole kwenye Msiba.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) na Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi wakiangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja dogo katika Kijiji cha Chang'ombe,linalounganisha Barabara inayotoka Kwarihombo kupitia Kwamsanja mpaka Kibindu,Kata ya Kibindu,ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 16,2014.


Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akipokea Jogoo kutoka kwa kina Mama wa Kijiji cha Kwamsanja,Kata ya Kibindu leo Machi 16,2014.
Mkutano ukiendelea.........








Mdau akisaka taswira Mwanana.
Wakimsikiliza kwa Makini Mgombea.

PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top