Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene akizungumza na wabahabari
(hawapo pichani) kuhusu utoaji wa Vitambulisho vya Waandishi wa Habari
kwenye shughuli za Bunge Maalum la Katiba.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene akizungumza na wabahabari
(hawapo pichani) kuhusu utoaji wa Vitambulisho vya Waandishi wa Habari
kwenye shughuli za Bunge Maalum la Katiba.Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi
wa Kitengo cha Vyombo vya Habari cha Idara hiyo, Vicent Tiganya.
Picha zote na Georgina Misama-MAELEZO
………………………………………………………………………………..
Na Frank Mvungi-MAELEZO
SERIKALI
imetoa ufafanuzi juu ya vitambulisho vya waandishi wa habari ( Press
card) wakati wa Bunge Maalum la katiba na kusema kuwa ndicho kigezo
pekee kitakachowezesha waandishi wa habari kutimiza majukumu yao vyema
katika kipindi chote cha bunge hilo.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari
Maelezo, Assah Mwambene wakati akitoa tamko la Serikali kufuatia
taarifa potofu zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa
nchini.
Mwambene
alibainisha kuwa utaratibu wa kutoa vitambulisho hivyo si mgeni kama
ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari na kwamba unaweza kukipata
ndani ya saa 24 ikiwa tu mwandishi anakidhi vigezo.
Alisema
vitambulisho vinatolewa tu kwa mwandishi mwenye taaluma ya uandishi wa
habari kutoka chuo kinachotambulika naSerikali kwa kuzingatia sheria na
kanuani zilizowekwa.
Alisisitiza kuwa utaratibu wa kutoa vitambulisho kwa waandishi habari upo na ni wa kisheria hivyo ni lazima ufuatwe.
Pia
alisema kuwa ni vyema kila mwandishi akafuata taratibu zote za kupata
kitambulisho kinachotolewa na MAELEZO kwa kuwa bila kitambulisho hicho
hataweza kufanya kazi katika kazi rasmi kama vile Bunge maalum la
katiba.
Alitoa
wito kwa waandishi wa habari kujiendeleza katika taaluma ya uandishi wa
habari kwa wale wasio na sifa za kupewa vitambulisho hivyo ili kuiniua
Sekta ya Habari hapa nchini.
Post a Comment