Afisa
Habari wa Wizara ya Viwanda na Uchukuzi, Nicodemas Mushi (kulia)
akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo
jijini Dar es Salaam kuelezea tamko la serikali kuanza ukaguzi wa
leseni za biashara. Pembeni yake ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Uhamasishaji Biashara na Masoko, Mashingo Christopher.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Uhamasishaji Biashara na Masoko, Mashingo
Christopher (kati) akikazia tamko la serikali juu ya ukaguzi wa leseni
za biashara. Pembeni yake ni Afisa Habari wa Wizara ya Viwanda na
Uchukuzi, Nicodemas Mushi (kushoto) na Afisa Habari wa Idara ya Habari
Maelezo, Frank Mvungi.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
Serikali
ilirejesha utaratibu wa kupata leseni ya biashara kwa kulipia kuanzia
1/7/2013. Wizara ilitoa kipindi cha miezi 6 kwa wafanyabiashara
waliokuwa na leseni zisizo na ukomo kuhuisha leseni zao.
Kipindi hicho cha miezi 6 kiliishia 31/12/2013.
Na
kama tulivyowatangazia Umma, wale waliochelewa kufanya hivyo walipata
leseni zao kwa kulipa ada na adhabu kwa mujibu wa Sheria ya Leseni Namba
25 ya 1972 kifungu cha 11(a) na (b).
Ukaguzi: (Kifungu na 17 cha Sheria Na 25 ya 1972)
Ukaguzi unafanyika ili kuhakikisha kuwa biashara zinafanyika kwa mujibu
wa Sheria na taratibu za nchi.
Kama
alivyoagiza KMWVB, kwamba Mamlaka za Leseni zifanye ukaguzi wa kina
katika maeneo yao, tunapenda kusisitiza kuwa ukaguzi huu ufanyike kati
ya mwezi wa Aprili na Mei.
Wito kwa wananchi
Wananchi kufuata Sheria na taratibu za nchi, kwani kufanya hivyo ni
alama ya maendeleo. Kigezo kimoja cha kupima maendeleo ya watu, ni kwa
jinsi gani watu hao wanafuata taratibu.
Post a Comment