“PRESS RELEASE” TAREHE 08.03.2014.
- WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUPINDUKA
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE WAKIWA NA POMBE HARAMU YA POMBE.
WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WENGINE WATATU KUJERUHIWA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUPINDUKA.
MNAMO
TAREHE 07.03.2014 MAJIRA YA SAA 10:00HRS ASAUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI
CHA KIWIRA, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE GARI
LENYE NAMBA ZA USAJILI T.985 BPC AINA YA TOYOTA DYANA LILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA WILLY AGENCY MANGUNGURU
UMRI KATI YA MIAKA 35-38, MKAZI WA KATUMBA–TUKUYU LILIMGONGA MTEMBEA
KWA MIGUU MARY ANYELWISYE (51) MKAZI WA KIJIJI CHA KIKOTA NA KUFARIKI
DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA MISHENI IGOGWE.
AIDHA MARA BAADA YA TUKIO HILO GARI LILIPINDUKA NA KUSABABISHA MAJERUHI
KWA ABIRIA WANNE WALIOKUWA NDANI YA GARI HILO KATI YAO REBY MWAIKENDA
(40) MKAZI WA RUNGWE ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU KATIKA
HOSPITALI YA MISHENI IGOGWE. MAJERUHI WALIOKUWEMO KATIKA GARI HILO NI
PAMOJA NA 1. LUGANO JANKEN (24) MKAZI WA KIKOTA 2. REO MWASEBA (74)
MKAZI WA KYELA NA 3. ALEX PHILIPO (25) MKAZI WA KATUMBA AMBAO WOTE
WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA MISHENI IGOGWE. CHANZO CHA AJALI NI
MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI. JUHUDI ZA KUMTAFUTA
ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA
MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA/KUFUATA SHERIA NA
ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA
TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE WAKIWA NA POMBE HARAMU YA POMBE.
WATU
WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. LATARO KASIUPA (42) 2. ULIMBOKA
MICHAEL (35) 3. SOPHIA ATUPELE (25) NA 4. VENUS OMARY (25) WOTE WAKAZI
WA IGURUSI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA
POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [05]. WATUHUMIWA
WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 06.03.2014 MAJIRA YA
SAA 17:00HRS JIONI HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA IGURUSI, TARAFA YA
ILONGO, WILAYA YA MBARALI. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA
KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI
KWA AFYA YA MTUMIAJI.
MTU ASIYEFAHAMIKA ATELEKEZA SILAHA HUKO KATIKA KIJIJI CHA UTAMBALILA.
MNAMO
TAREHE 07.03.2014 MAJIRA YA SAA 10:45HRS ASUBUHI JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA LIKIWA KATIKA MSAKO HUKO KATIKA KIJIJI CHA UTAMBALILA, KATA YA
NAMBINZO, TARAFA YA ITAKA, WILAYA YA MBOZI LILIFANIKIWA KUKAMATA SILAHA
MOJA BUNDUKI AINA YA GOBOLE INAYOTUMIA RISASI ZA GOROLI IKIWA
IMETELEKEZWA KWENYE PAGALA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KWA JESHI LA POLISI JUU YA
MTU/WATU WANAOMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA ILI WAKAMATWE NA
KUFIKISHWA MAHAKAMANI, VINGINEVYO WASALIMISHE WENYEWE SILAHA HIZO.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment