Katibu
Mtendaji wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM)
Tanzania Rehema Twalib (wa kwanza kushoto) akiongea na waandishi wa
habari leo jijijni Dar es salaam ambapo Tanzania inaungana na nchi
nyingine za Afrika wanachama wa mpango huo kuadhimisha siku APRM na
kutoa taarifa ya tathmini ya utawala bora nchini. Katikati ni Afisa
Habari Idara ya Habari MAELEZO Frank Mvungi na wa kwanza kulia ni
Mratibu wa APRM Tanzania Dkt. Cuthbert Ngalepeka.
Katibu
Mtendaji wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM)
Tanzania Rehema Twalib (wa kwanza kushoto) akiongea na waandishi wa
habari leo jijijni Dar es salaam kuhusu hatua zilizofikiwa na Serikali
ya Tanzania kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa mkataba wa Afrika wa
tathmini ya APRM. Pamoja kuzungumzia masuala ya kitaifa hususani
mchakato wa katiba unaoendelea. Wa kwanza kulia ni Afisa Habari Idara ya
Habari MAELEZO Frank Mvungi.
Katibu
Mtendaji wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM)
Tanzania Rehema Twalib (wa pili kushoto) akiongea na waandishi wa habari
leo jijijni Dar es salaam ambapo alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa
nchi 34 kati ya 54 zilizojiunga na mpango wa APRM na kuwashirikisha
wananchi kutoa maoni yaokuhusu hali ya utawala bora nchini. Wa kwanza
kushoto ni Afisa Mawasiliano wa APRM Hassan Abbasi.

…………………………………………………………………………………………..
Na Frank Mvungi-MAELEZO
MPANGO
wa Afrika wa kujitathmini kiutawala bora (APRM) umebainisha kuwa
Tanzania ni moja ya Nchi zinazofanya vizuri katika utawala bora.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mtendaji wa APRM Tanzania Rehema Twalib wakati wa
mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam alipokuwa
akieleza mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa ikiwa ni sehehmu ya
maadhimisho ya siku mchako huo ambayo huadhimishwa Machi 9 kila mwaka.
Bi
Rehema alibainisha kuwa Tanzania imepata mafanikio katika Nyanja za
Demokrasia na Utawala Bora, Siasa, Usimamizi wa uchumi, uendeshaji wa
makampuni,Maendeleo ya uchumi-Jamii na Masuala mtambuka kama afya.
Akifafanua
zaidi Bi. Rehema alisema Tanzania kupitia APRM imefanya tathmini yake
katika maeneo hayo na kuwasilisha ripoti yake mbele ya wakuu wa nchi
wanachama na kujadiliwa.
Wakati
huo huo alizitaja hatua zinazochukuliwa na Serikali kuwa ni kuanza
kufanyia kazi mpango kazi wa kitaifa (NPoA) wa kuondoa changamoto
zilizobainishwa katika ripoti ya APRM kuhusu hali ya utawala bora
nchini.
Pia
Bi Rehema alizitaja hatua nyingine ambazo Tanzania imefikia
katikakutekeleza mchakato wa APRM kuwa ni kuwashirikisha wananchi kutoa
maoni yao kuhusu hali ya utawala bora nchini na Serikali kuruhusu
wataalamu wa utawala bora kutoka nchi wanachama kuja nchini kuhakiki
mchakato huo.
Aidha,
Bi Rehema alibainisha kuwa lengo kuu la mpango huu ni kuwashirikisha
wananchi ili kushirikiana na Serikali zao kubaini changamoto za utawala
bora ili zifanyiwe kazi na kuhimiza nchi kutekeleza viwango
vinavyokubalika kimataifa na kikanda.
APRM
ni mpango ulioasisiwa machi 9, 2013 na wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika
(AU) ambapo Tanzania kwa sasa ni miongoni mwa nchi 34 kati ya 54 za AU
zilizokwisha jiunga na mpango huu ambapo ilijiunga mwaka 2004.
Post a Comment