Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za
kifo cha mshabiki wa soka anayedhaniwa kuwa ni wa Yanga, Deodatus
Mwakyangula kilichotokea jana (Machi 19 mwaka huu) wakati ya mechi kati
ya Yanga na Azam iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Msiba
huo ni mkubwa kwa familia ya Mwakyangula na kwetu, kwani umetokea
wakati akiwa uwanjani kushuhudia mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Mwakyangula, na klabu ya Yanga na
kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha
msiba huo mzito.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina
Post a Comment