Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Tujivunie Uimara wa Muungano wetu-BALOZI LUSINDE

 

      
SONY DSC
Wananchi wa Tanzania wamepongezwa kwa kufikia miaka 50 ya Muungano huku  wakiulinda na kuuimarisha mpaka Leo.
Hayo yamesemwa na Balozi Job Lusinde ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya kutayarisha katiba ya Muungano Hivi karibuni Mjini Dodoma.
Balozi Lusinde ambaye pia alikuwa Waziri  wa  serikali za Mitaa katika Baraza la kwanza la  Tanganyika mwaka 1961, baada ya kupata Uhuru amesema  kwamba madhumuni ya kuanzisha Muungano huo ilikuwa ni kuonyesha  mfano ili siku moja uwepo Umoja wa nchi za Afrika.
“Wakati  tunaugana na Zanzibar kulikuwepo upepo wa kuwa na Shirikisho la Afika Mashariki, hivyo ilikuwa rahisi kuanza na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Kama mfano mkubwa wa kimatendo ” alisema Balozi Lusinde.
Aliendelea kusema kwamba madhumuni mengine yalikuwa ni kuuimarisha uchumi  wa nchi hizi mbili kwani kabla ya Muungano Zanzibar ilikuwa na watu 300 na Tanganyika ilikuwa na watu 8,000,000, hivyo baada ya kufunga na uchumi ukiwa unategemeana na wakaunganisha nguvu kiuchumi , jambo ambalo lilikuwa faida kwa nchi hiyo mbili.

Aidha, Balozi Lusinde alisema kwamba  wakati wa kuungana walifikiria suala la usalama wa nchi hizi mbili, kwamba ni muhimu hivyo kwa kuungana kutaweza kuimarisha usalama.
Suala la mwingiliano wa kijamii pia lilichochea kuungana kwa nchi hizi mbili. “kulikuwa na mwingiliano mkubwa awa kijamii kama vile kuoleana, kutembelea a na biashara,  hivyo kutokana na Wazanzibar kuishiTanganyika na halikadhalika Watanganyika kuishi Zanzibar, suala la kuungana lilikuwa Kama liko tayari” alisema Balozi Lusinde.
Aliongeza kusema kwamba baada ya Muungano, umoja, usalama na uchumi uliimarika.
Balozi Lusinde alisisistiza suala la kuulinda na kuuimarisha Muungano wetu na kushauri changamoto zilizopo zizungumzwe na kutafutiwa ufumbuzi.
Akizungumzia uwepo wa Serikali tatu, Balozi LUsinde alisema Hanoi haja ya kuwepo maana miaka 50, ya Muungano tunaona matunda yake.”serikali tatu hazina haja ya kuwepo, kwani zitaleta katika uendeshaji wake, pili serikali hizi zitakuwa na gharama ya uendeshaji wake,  na tatu zitawachanganya wananchi” aliongeza Balozi Lusinde.
Balozi Lusinde aliendelea kusema kwamba serikali tatu ni sawa sawa na kuweka gia ya kumrudi nyumbani kwenye gari na kwamba serikali tatu zitatupeleka kwenye uharibifu na kutusambaratisha.
Balozi Lusinde alimalizia kwa kushauri kwamba  Muungano wetu  usiwekewe kitu chochote cha kuwavuruga Watanzania ili wasivurugike, wasitengane na wasigombane.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top