Jay-z ana utajiri unaokadiriwa dola millioni 475 za
kimarekani kwa takwimu za mwaka 2013. Mafanikio ya jay-z yamefikiwa kwa
kiasi kikubwa kwa biashara anazofanya.Kufanya zaidi, Kujitoa zaidi na
kuona zaidi ndio kinachomfanya jay-z azidi kusimama kama nguli hatari
wa muziki, fashion excecutive na mkali wa burudani. Ukiongelea
Jay-z kama Jay-z basi unaweza kutumia mstari kutoka kwenye nyimbo ya
kanye west “Diamonds From Sierra Leone”: “I’m not a businessman, I’m a business, man!” yaani
ikimaanisha yeye sio mfanyabiashara bali yeye mwenyewe ndio biashara.
Hiki ndio kitu kilichokosekana hapa bongo, msanii kubadilisha mtazamo
wake kama anafanya biashara na kuanza kuji-brand mwenyewe kama
biashara. Hivi sasa Diamond ndio msanii pekee ambayo anaweza kubadilisha
vitu kadhaa na kufika level alizopo Jay-z na hivi ndivyo vitu vya
kufanya ;-
Kua mtafutaji zaidi
Kabla Shawn Carter ajawa Jay-Z, akiwa na miaka 12 alikua akiuza
madawa ya kulevya maeneo ya Marcy Projects , maeneo hatari sana
huko Brooklyn. Japokua jay-z hakuwa anafanya kitu kizuri lakini ule moyo
wa
kutafuta ndio umemfanya afike alipo sasa. Japokua Diamond ana
historia kidogo kama jay-z sababu naye mwaka 2008 na 2009 alikuwa
akifanya kazi katika kiwanda cha mabegi kilichoko Mikocheni na kulipwa
mashahara wa shilingi 2,000 kwa masaa 8, huku nauli ikimgharimu shilingi
1,000 mpaka kufika kwao na hapo chakula ni zaidi ya shilingi
1,000.Ameshauza maji hadi mitumba . Somo ambalo amejifunza jay-z
akifanya biashara mtaani ni kutompa mtu discount , kama aliuza kitu kwa
dola 10 basi hawezi kupunguza iwe dola 9.95 hata kama ni rafiki yake wa
karibu. Hiki ni kitu kinachowafanya wasanii wengi wasifanikiwe hasa
wasanii wakubwa. Katika kitabu chake cha decoded jay-z alisema
“Nilioamua kujiingiza katika rap, sikuwa nimeweka kiapo cha
umaskini,niliona ni nafasi nyingine ya kupigana, nafasi ambayo inaendana
na kipaji changu halisi cha muziki.nilikua msanii mwenye hamu na mwenye
kusita pia,lakini umuhimu wa ninachotaka kufanya ndio ulisababisha
mambo yote yafanikiwe, inabidi uwe msanii usiyebadilika”
Kutengeneza opportunity zako mwenyewe
Kwa jay-z mafanikio hayakua tu kuchukua opportunities zilizokwepo,
ilikua ni kutengeneza opportunity zake mwenyewe. Jay-z alipoanza kurap
kulikua hakuna label ambazo zilikua tayari kumchukua kwahiyo
akaamua kushirikiana na Damon Dash and Kareem Burke kutengeneza label
yake mwenyewe ya , Roc-A-Fella Records. Inashangaza kwa mafanikio
aliyonayo diamond kwasasa ameshindwa hata kuanzisha recoring label yake
mwenyewe na kutegemea kila siku kusumbuka kwenye label za watu wengine.
Jay-z pia alikua ni mpenzi wa fashion hasa brand ya Iceberg Apparel ya
italia aliamua kushirikiana na Dash na kuanzisha brand ya nguo za
Rocawear, ambayo aliiuza baadae kwa $204 million. Diamond sasa ameanza
biashara ya nguo lakini inaonekana kutovutia watu wengi so inabidi
ajipange kuja na brand moja hatari.
Kuwa power couples
Jay-z na beyonce ndio celebrity couples wanaoongoza kuingiza pesa
nyingi duniani kutokana na takwimu zilizofanywa na forbes. Kama
tunavyojua unaweza kujiita mwenye bahati kama utaweza kuspend siku nzima
ofisini na partner wako bila ya kurushiana stepler. lakini Beyonce na
Jay-z wanaweza kujihesabia kama wenye bahati kwasababu wameweza kufanya
kazi pamoja na kuwaingizia dola za kimarekani millioni 95 mwaka jana.
Wema Sepetu na Diamond Platnumz ndiyo super couples pekee iliyopo bongo,
tumeona wakituonesha malavidavi lakini katika maswala serious ya
kuingiza mshiko hawajaweza kutumia kigezo hicho kujitajirisha.Sasa ni
wakati muafaka wa diamond kutulia na wema sepetu na kuangalia
watatumiaje umaarufu wao kuingiza mshiko kama wanavyofanya jay-z na
beyonce .
Post a Comment