Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki akizungumza na waandishi
wa habari leo jijini Dar es salaam kutoa agizo kwa viongozi na watendaji
wa jiji la Dar es salaam kuhakikisha kuwa wanawaondoa na kuwachukulia
hatua za kisheria wanaovunja sheria za jiji kwa kuendesha shughuli
mbalimbali katika maeneo yasiyoruhusiwa.Kamanda
wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna (CP) Suleiman Kova akitoa
ufafanuzi ameeleza kwa waandishi wa habari kuhusu wakazi wa jiji la Dar
es salaam hususan madereva wa bodaboda na Bajaji kufuata sheria za
barabarani na kajenga tabia ya kufanya tathmini ya safari zao iwapo
wanakidhi vigezo vya usalama barabarani ili kuepusha madhara.Afisa
Mfawidhi wa SUMATRA Kanda ya Mashariki Bw. Conrad Shio akitoa ufafanuzi
kwa waandishi wa habari kuhusu sheria inayosimamia usafiri wa Bajaji
na Bodaboda nchini.
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Dar es salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki amewaagiza viongozi na
watendaji wa jiji la Dar es salaam kuhakikisha kuwa wanawaondoa na
kuwachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha
mahakamani wakazi wa jiji la Dar es salaam wanaovunja sheriaza jiji kwa kuendesha shughuli mbalimbali katika maeneo yasiyoruhusiwa.
Aidha
amewataka waendesha pikipiki maarufu kwa jina la “Bodaboda”, Bajaji,
waendesha baiskeli na mikokoteni wanaofanya biashara ya kubeba abiria na
mizigo maeneo yasiyoruhusiwa kisheria kuondoka wenyewe kabla hatua kali
za kisheria hazijachuliwa dhidi yao.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Saidi Mecki Sadiki amesema kuwa jiji la Dar es salaam limeamua
kuchuakua uamuzi huo kufuatia tatizo la baadhi ya wananchi kuamua
kuvunja sheria zilizowekwa kwa kisingizio cha ugumu wa maisha na
kutafuta fedha hali inayoleta usumbufu kwa wananchi wengine .
Amesema
kuwa licha ya changamoto inayolikabili jiji la Dar es salaam hasa
maeneo ya katikati ya mji hali iliyopo sasa ya biashara holela na
uvunjifu wa sheria unaofanywa na maendesha Bodaboda, Bajaji, baiskeli,
mikokoteni na Taxi bubu maeneo yasiyoruhusiwa kisheria hauwezi
kuvumilika.
“Jiji
la Dar es salaam tumekuwa na kero ya muda mrefu hasa ya omba omba,
waendesha baiskeli, bodaboda na wafanyabiashara katika maeneo ya
makutano ya barabara katika maeneo yasiyoruhusiwa hali hii hatuwezi
kuivulimia, sisi hatufukuzi watu bali tunawataka wafuate sheria za jiji”
Amesisitiza.
Ameeleza
kuwa serikali haina lengo la kuwazuia wananchi kufanya biashara na
shughuli nyingine za kujiingizia vipato kama wanazingatia sheria na
taratibu zilizowekwa na kuongeza kuwa wale wote wanaoomba leseni za
kufanyia biashara wanapewa taratibu na miongozo na masharti ya
kuzingatia wanapofanya biashara zao jambo ambalo wengi wao wanashindwa
kulizingatia.
“Kila
Manispaa ina miongozo na kanuni za uendeshaji wa shughuli zake ikiwa ni
pamoja na mamlaka ya kutenga maeneo ya biashara na kuwaruhusu wale
wanakidhi masharti ya leseni zao kufanya biashara zao ila wengi wao hasa
madereva wa Bajaji na Bodaboda hawazingatii haya” Amesisitiza Mh.
Sadiki.
Ameeleza
kuwa sheria zote zilizotungwa zimewekwa ili zifuatwe kwa ustawi wa
taifa na si vinginevyo na kubainisha kuwa wote waliovamia maeneo ya
vituo vya mabasi, maeneo ya vituo vya umeme na hifadhi za barabara ni
vema wakaondoka wenyewe na kukubali kutii sheria bila shuruti huku
akitoa mfano wa baadhi ya wafanyabiashara na wauza vyakula “mama lishe”
walio anza kuvamia maeneo ya ujenzi wa mradi wa mabasi yaendayo Kasi
(DART).
“Haiwezekani
sheria za jiji zikavunjwa na sisi tukaendelea kuwaangalia baadhi yao
wamefikia hatua ya kuvamia maeneo ya mradi wa mabasi yaendayo kasi na
kuanza kufanya biashara na kuwasumbua mafundi jambo lisilokubalika”
Akizungumza
kuhusu biashara ya bodaboda inayofanywa na vijana walio wengi jijini
Dar es salaam Mh. Sadiki ameeleza kuwa mpango wa serikali kuruhusu
Bodaboda na Bajaji kutumika kubebea abiria ulikuwa na maana nzuri ya
kuwawezesha wananchi kupata usafiri hasa katika maeneo yasiyofikika
kirahisi kwa magari hasa vijijini na kuongeza kuwa utakua na mafanikio
kama watafuata sheria.
‘Serikali
iliruhusu usafiri wa Pikipiki na Bajaji kutumika kubebea abiria kwa nia
nzuri ikiwa ni pamoja na kurahisisha usafiri na kuongeza ajira,hivyo
siyo nia yetu kuwadhalilisha vijana hawa tunachowataka wafanye ni
kufuata sheria za nchi”
Aidha
kwa upande wa ongezeko la ombaomba ambao baadhi yao walirudishwa katika
maeneo yao ya awali na kurejea tena jijini Dar es salaam ameeleza kuwa
utaratibu wa kuwafuatilia uko pale pale na kufafanua kuwa watakaokutwa
na makosa ya kukaa maeneo yasiyoruhusiwa watafikishwa mahakamani.
Kwa
upande wake Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna (CP)
Suleiman Kova ameeleza kuwa ni wakati sasa wa wakazi wa jiji la Dar es
salaam hususan madereva wa bodaboda na Bajaji kufuata sheria na
kusisitiza kuwa ni vema wananchi wakajenga mazoea ya kufanya tathmini ya
safari zao iwapo wanakidhi vigezo vya kuwawezesha kutembea barabarani.
“Kwa
waendesha pikipiki “bodaboda” hali ni mbaya wengi wameumia na kupata
ulemavu wa kudumu kwa kutozingatia sheria za usalama barabarani na
kukidhi matakwa ya kuendesha pikipiki hizo”
Amesema
kuwa Jeshi la Polisi litafanya kazi yake kwa kushirikiana na manispaa
zote tatu kuhakikisha kuwa vitendo vya uvunjifu wa sheria vinakomeshwa
na kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa pindi wanapoona dalili zozote
za uvunjifu wa amani hasa matukio ya ujambazi kwa kutumia pikipiki
yayoendelea kuongezeka kwa kasi.
“Napenda
niwahakikishie wananchi kuwa jeshi la polisi tumejipanga vizuri
kukabiliana na vitendo vyote vya uhalifu wa aina zote, pia natoa wito
kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam hasa wafanyabiashara kuepuka
kutembea na fedha nyingi ili kuepuka madhara ya kuvamiwa”
Naye
Afisa Mfawidhi wa SUMATRA Kanda ya Mashariki Bw. Conrad Shio ameeleza
kuwa sheria ya usafirishaji kusimamia Bajaji na Bodaboda iko wazi na
kuongeza kuwa serikali ina wajibu wake na pia waendesha pikipiki na
Bajaji wanawajibu wao wa kuzingatia kanuni taratibu na kanuni
zilizowekwa.
“Sisi kama SUMATRA tunaendelea kufanya kila tuwezalo kukabiliana na vitendo vyote vya uvunjivu wa sheria za barabarani”
Post a Comment