Maisha, majukumu, uzazi na mambo mengine, yamewafanya wasanii
wengine kuacha muziki na kuendelea na shughuli zingine zikiwemo za
ujasirialimali ama za ofisini. Wengine wameacha baada ya kuona pamoja na
kufanya muziki mzuri, kile kinachopatikana hakiwezi kufuta jasho la
jitihada zao na kwakuwa maisha lazima yaendelee. Bahati mbaya ama nzuri,
baadhi ya wasanii waliacha muziki wakiwa bado kwenye peak na hivyo
kufanya kuwa na ‘demand’ kubwa ya nyimbo zao mpya kwa mashabiki wao.
Jacqueline Ntuyabaliwe aka K-Lyinn
Wakati K-Lyinn anafanya muziki, hakuna ubishi ndiye alikuwa
mwanamuziki mrembo zaidi nchini Tanzania. Pengine ilikuwa ni surprise
kwa wengi nikiwemo mimi niliyekuwa namfahamu zaidi kwa nafasi ya Miss
Tanzania (2000) kubaini kuwa kumbe ni mwanamuziki mzuri pia.
Lakini kile ambacho nilikuwa sifahamu ni kwamba K-Lyinn alianza kuimba hata kabla ya kushinda taji hilo.
Alianza muziki kwa kuimba na bendi ya Tanzanites ambako alikuwa muimbaji mkuu kwa miaka mitatu. Akiwa na bendi hiyo aliwahi kufanya ziara katika sehemu mbalimbali duniani zikiwemo Dubai, Bahrain na Abu Dhabi.
Alianza muziki kwa kuimba na bendi ya Tanzanites ambako alikuwa muimbaji mkuu kwa miaka mitatu. Akiwa na bendi hiyo aliwahi kufanya ziara katika sehemu mbalimbali duniani zikiwemo Dubai, Bahrain na Abu Dhabi.
Mwaka 2004 aliachia album yake ya kwanza ikiwa na hit kama “Nalia Kwa
Furaha” aliyomshrikisha Bushoke. Wimbo huo ulifanya vizuri mno na hadi
sasa video yake inabaki kuwa miongoni mwa video za muziki za wasanii wa
Tanzania zilizoangaliwa sana kwenye Youtube ikiwa na views zaidi ya
1,303,080. Pia kwa miaka 7 iliyopita, hakuna ubishi ilikuwa ni video
bora kabisa kwa Tanzania na pengine urembo wake ulifanya video ivute
attention ya watu wengi.
Nalia Kwa Furaha haikumfanya K-Lyinn kuwa ‘one hit wonder’ kwakuwa
baada ya miaka mitatu alikuja kutawala tena mawimbi ya redio kwa wimbo
wake ‘Crazy Over You’ aliomshirikisha Squeezer. Video yake pia
ilitengeneza muelekeo mwingine wa video bora za muziki za Tanzania na
tena urembo wake kwenye video hii ulivutia wengi.
Hakuishia hapo tena, K-Lyinn aliendelea kuachia hits nyingine kibao
ukiwemo ‘Chochote Utapata’ aliomshirikisha rapper wa Chamber Squad,
Noorah aka Babastylez.
“Kwa mimi ninavyomuona ni mtu aliyekuwa anajua nini anachotaka kufanya,” anasema Noorah.
“Wimbo ulipokelewa vizuri sana yaani, tofauti na nilivyokuwa natarajia, sikudhani kama ungekuwa mkubwa.”
Noorah anasema hadi sasa K-Lynn ana mashabiki wengi wanaomhitaji
arudi tena. “Mashabiki ni watu ambao wana nguvu yao kubwa sana. Unaweza
ukawa umefanya nini, sijui umefikia wapi kwenye maisha yako lakini
mashabiki kama wamekupenda, wamekupenda tu na mimi kimtazamo wangu naona
walimpenda sana, kwa mapenzi waliyokuwa nayo juu yake, obvious bado
wanamuhitaji.”
Mr Blue ni msanii mwingine aliyeshirikishwa na K-Lyinn kwenye wimbo wake ‘Nipe Mkono’ ambao nao ulifanya vizuri.
“Mara ya kwanza nilimuona akiwa anahojiwa na nikamsikia akisema ‘bana katika watu ninaopenda kufanya nao kazi ni Mr Blue, tukifanya kazi pamoja itakuwa ni vizuri,” anasema Blue.
“Mara ya kwanza nilimuona akiwa anahojiwa na nikamsikia akisema ‘bana katika watu ninaopenda kufanya nao kazi ni Mr Blue, tukifanya kazi pamoja itakuwa ni vizuri,” anasema Blue.
“Mwisho wa siku akanipigia simu na tukaonana ndio tukaifanya hiyo
kazi pamoja. K-Lyinn ni mtu anayejituma, anafuatilia kazi yake kwa
makini na nini, mimi nashauri ni vizuri akirudi. Kama alifanya kwaajili
ya mashabiki basi asiwaache njia panda. Siwezi kusema anafanya kwaajili
ya pesa atakuwa hana shida, lakini kama atafanya kwaajili ya mashabiki
aendelee tu.”
Ni kweli K-Lyinn hana shida kwakuwa kwa sasa ni mchumba wa miongoni
mwa watu matajiri zaidi barani Afrika kwa mujibu wa Forbes, Mwenyekiti
Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi ambaye wamejaaliwa watoto mapacha wa
kiume. Pamoja na hivyo, Jacky ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni yake ya
mapambo ya ndani, Amorette Ltd.
Kuna uwezekano akarejea tena kwenye muziki? Sio rahisi. Baada ya
kuulizwa sana swali la kwanini aliacha muziki, June mwaka jana, K-Lyinn
aliitaja sababu.
“Huwa naulizwa sababu ya kuacha muziki,mojawapo ilikua ni
ukandamizwaji na kutopewa haki kama msanii.Natumaini waliobaki
watapigania haki,” alitweet K-Lyinn.
Kwakuwa Miss Tanzania huyo wa zamani aliacha muziki akiwa kwenye
peak, bado anachukuliwa kama miongoni mwa wasanii bora wa kike kuwahi
kutokea nchini na ana mashabiki wengi.
Kazi zake zingine..
Besti
Nikipata Wangu
Post a Comment