Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wajumbe wa Bunge Maalum wasusia Bunge


Wakati Bunge Maalumu la Katiba linatarajia kuanza kujadili Rasimu ya Katiba kesho, baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo wameanza kuondoka bungeni, kupinga mwenendo wa Bunge hilo.

Hatua hiyo ya wabunge hao inakuja wakati Bunge Maalumu la Katiba juzi lilipitisha azimio la kutumia kura ya siri na wazi katika kuamua vifungu vya rasimu.


Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samia Saluhu alisema baada ya kupitishwa kwa utaratibu wa kupiga kura za siri na wazi katika Bunge hilo, kuanzia Jumatatu wataanza kujadili sura ya kwanza na sita ambayo inahusu Muundo wa Muungano.

Katika sura ya kwanza, mambo ambayo yanatakiwa kujadiliwa ni Jina, Mipaka, Alama, Lugha na Tunu za Taifa wakati sura ya sita mambo ambayo yanapaswa kujadiliwa ni Muundo wa Muungano.

Lema atangaza kurudi jimboni Arusha

Mjumbe wa Bunge hilo, Godbless Lema alisema anakusudia kuondoka bungeni, kutokana na kutoridhishwa na maridhiano ya kupiga kura za siri na wazi katika kufikia uamuzi katika Bunge hilo.

Akizungumza na Mwananchi jana, Lema alisema hakubaliani na utaratibu uliopitishwa, kwani unalenga kulazimisha kila jambo ambalo chama tawala kinalitaka lipitishwe.

“Huu utaratibu wa kura kupigwa kwa wazi na siri katika kitu kimoja, haupo sehemu yoyote duniani. Sasa sisi kukubali ni kuwasaliti wananchi, kwani hata Dodoma tunaandaa rasimu ya Katiba ya wananchi wote siyo ya CCM pekee,” alisema Lema.

Alisema pia hakubaliani na utaratibu wa kujadili rasimu ya Katiba, ambao umetolewa na Kamati ya Uongozi kwa kuanza na sura ya kwanza na ya sita, kwani vinalenga kufumua Rasimu ya Jaji Warioba.

“Hapa CCM wanataka kulazimisha Serikali mbili kwa kujadili kwanza vifungu hivi, kama vitapita basi watakuwa na uwezo wa kubadili rasimu yote kitu ambacho mimi siwezi kukaa kwenye Bunge hili na kusaliti wananchi waliotoa maoni kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba,” alisema Lema.

Jussa atabiri Bunge kuvunjika.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mjimkongwe, Ismail Jussa, alisema uchaguzi wa vifungu hivyo ambavyo ndivyo vinabeba Rasimu ya Katiba, vinaashiria kuvunjika kwa Bunge hilo katika hatua za awali.

SOMA ZAIDI ..http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Wajumbe-wa-Bunge-Maalum-wasusia-Bunge/-/1597296/2262744/-/14vdfrkz/-/index.html
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top