Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa akifungua mkutano wa siku ya wadau wa
Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la
mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA
inavyofanya kazi. Kikao hicho kimefanyika leo Machi 28, 2014 katika
ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni Mkuu wa Wilaya ya
Korogwe, Mheshimiwa Mrisho Gambo (kushoto) na Mwenyekiti wa Hamashauri
ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello
Bendera (kulia).
Mkuu
wa Wilaya ya Korogwe, Mheshimiwa Mrisho Gambo akitoa ufafanuzi wa jambo
mbele ya mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa (kushoto). Pembeni
ni Diwani wa Kata ya Mgombezi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu,
Afya, Maji na Uchumi, Mheshimiwa Omari Chafesi na Meneja wa Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu
(kushoto).
Meneja
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally
Mwakababu akieleza umuhimu wa matumizi ya Tiba kwa Kadi (TIKA) mbele ya
mkuu wa mkoa wa Tanga.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole,
Mheshimiwa Angello Bendera (kushoto) akiendesha mkutano wa siku ya wadau
wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo
la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA
inavyofanya kazi. Pembeni ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa
Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji
Korogwe, Dokta Jerry Mwakanyamale.
Post a Comment