Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii,Seif Rashidi akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam, kuhusu maadhimisho ya wiki ya afya ya
Figo itakayoanza tarehe 10 hadi 14, na kuadhimishwa kitaifa tarehe 13
mjini Dodoma katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, kauli mbiu ya
maadhimisho hayo ni “Figo huzeeka , kadiri mtu anavyozeeka. Jali afya ya
Figo zako”.( Lorietha Laurence-Maelezo)
Na Lorietha Laurence-Maelezo
Asilimia
1.03 ya vifo hutokana na ugonjwa wa figo, hayo yalisemwa na Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii Seif Rashidi alipokuwa akitoa tamko kwa
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam,kuhusu siku ya afya ya
figo itakayoadhimishwa tarehe 13 Machi,mwaka huu mjini Dodoma.
Kauli
mbiu ya maadhimisho hayo “Figo huzeeka, kadiri mtu anavyozeeka. Jali
Afya ya Figo zako”. Lengo ni kuelimisha jamii ili iweze kuelewa umuhimu
wa figo katika mwili, watu kubadili staili za maisha,
kuhamasisha watoa huduma kuhusu wajibu wao katika kugundua magonjwa ya
figo na kupunguza hali hatarishi za ugonjwa sugu wa figo na kuandaa
mikakati madhubuti ya kukinga na kuthibiti magonjwa ya figo.
“
Nawasihi watu wawe na taratibu za kufanya vipimo mara kwa mara, pia
kujali afya zao kwa kuwekeza katika maendeleo ya afya zao ili kujikinga
na ugonjwa wa figo” alisema Mhe.Rashidi .
Aliongeza
kuwa ugonjwa huo husababishwa na shinikizo la damu,ugonjwa wa kisukari
na kutokufanya mazoezi mara kwa mara,msongo wa mawazo,unywaji pombe,
unene uliokidhiri,ulaji usiofaa , matumizi ya chumvi na mafuta pamoja na
uvutaji sigara.
Alifafanua
kuwa ugonjwa huo unaweza kumuathiri mtu yeyote aliye katika umri
wowote, ingawa hujitokeza zaidi kwa watu wenye umri wa miaka 50, ambapo
takwimu zinaonyesha kuwa kati ya mwanaume mmoja kati ya watano na
mwanamke mmoja kati ya wanne wenye umri wa miaka 65 hadi 74 wana ugonjwa
wa figo.
Pia
alieleza kwamba figo ni kiungo muhimu katika mwili wa binadamu,
husaidia katika kuchuja na kuondoa taka mwilini ,majimaji yaliyozidi
na kudhibiti kiwango cha kemikali mwilini kwa kudhibiti shinikizo la
damu.
Aliwataka watu
waepukane na ugonjwa huu wa figo, kwa kufuata ushauri wa wataalama
na kuzingatia mazoezi, kunywa glasi 6 hadi 8 za maji kwa siku,kuepuka
matumizi ya sigara na bidhaa zinazotokana na tumbaku, kuzingatia
maelekezo ya wataalam, kutumia dawa kwa usahihi na kufuatilia kiwango
cha sukari mwilini.
.
Maadhimisho
ya afya ya figo duniani yalianza mwaka 2006,ambapo mwaka huu
yataadhimishwa kuanzia tarehe 10 hadi 14 Machi, katika viwanja vya
Mwalimu Nyerere mjini Dodoma,shughuli zitakazofanyika ni pamoja na kutoa
huduma ya kupima afya ya figo,kutoa ushauri nasaha na kutoa tiba na
rufaa.
Post a Comment