Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZEE WA KURA ZA SIRI NA MICHEPUKO WAMTOSA MGOMBEA WAO CHALINZE SOMA HABARI KAMILI LIVE HAPA!!


CHADEMA YAMTOSA MATHAYO THORONGEY

Chama cha demokrasia na maendeleo "CHADEMA" kimemtosa mgombea wa ubunge wa jimbo la Chalinze Mathayo Thorongey richa ya upinzani mkali anaouonyesha dhidi ya Ridhwan Kikwete "mgombea wa magamba"

Habari toka ndani ya chadema zinasema kua Chama kimeshindwa hata kufanya mawasiliano kwenye vyombo vya habari ili baadhi ya mikutano irushwe kupitia taarifa mbalimbali za habari kama ilivyokua Kalenga na maeneo mengine yaliyokua na chaguzi za marudio
.

Habari zaidi zinaeleza kua mpaka sasa hakuna kituo chochote cha matangazo ya luninga kilichorusha japo mkutano mmoja wa chadema Jimbo la chalinze, tofauti na Ilivyokua Kalenga ambako kila mkutano uliripotiwa kupitia television kadhaa nchini.

Pia katika kampeni za Kalenga timu yote ya kampeni ilikua ikilipwa sh elfu 40, kwa siku kwa ajili ya kujikimu kwa chakula na malazi, lakini Chalinze watu wanaambiwa wajitegemee kwa kila kitu hali iliyopelekea wengi kushindwa kujikimu na kurudi makwao kufanya majukumu mengine ya kimaisha.

Taarifa za kuaminika zinaeleza kua kuna baadh ya viongozi wa chadema wakiwemo mratibu wa kanda ya Pwani "Nickson Tugala" na Katibu wa mkoa wa Kinondoni "Henry Kilewo" wamechukua fedha kutoka kwa Ridhwan Kikwete kupitia Kwa dada anayejulikana kwa jina la Olivia na kiasi cha pesa kilichotolewa ni sh 8.5ml. Kama fedha za awali na zingine zitatolewa siku moja kabla ya uchaguzi, kazi ya pesa hizo ni kuhakikisha wanapitisha majina ya mawakala wa ccm kwa kivuli cha chadema ili wakaibe kura za Mathayo hasa kwa maeneo ambayo mathayo anakubalika na wapiga kura.

Kwa kuamini hilo tayari mawakala feki wengi wamepelekwa kupitia kwa viongozi wa Chadema ni msingi, program inayosimamiwa na mratibu huyo hali ya kua kuna viongozi wa majimbo na wilaya, kwa nini viongozi hao wasitumike kutafuta mawakala?

HUU NI MWENDELEZO WA VITENDO VYA MRATIBU WA KANDA KUIMALIZA CHADEMA TARATIBU NA SAFARI HII AKISHIRIKIANA NA HENRY KILEWO.

Source: Rafiki wa karibu wa Mathayo.
— at New Dodoma Hotel.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top