Msanii
 wa Bongo Movie, Wema Sepetu na pia alikuwa ni jaji wa shindano la 
kusaka vipaji kwa watoto waliokuwa na umri kuanzia miaka minne(4) mpaka 
kumi na tano (15) akizungumza na mshiriki wa shindano hilo la kusaka 
vipaji kwa wanaojua kuigiza. Shindano hili limefanyika leo kwenye 
viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam na kuwapata watoto watatu 
waliokuwa wanaitajika.
Jaji
 Wema Sepetu akiwa na Jaji mwenzake Aunt Ezekiel walipokuwa wanawafanyia
 usahili watoto waliofika kwenye shindano la kusaka vipaji vya watoto 
wanaoweza kuigiza.
Msanii
 wa Bongo Movie, Wema Sepetu akicheza muziki na mmoja wa washiriki wa 
shindano  la kusaka vipaji lililofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders.
Director wa shindano la kusaka vipaji, Adam akizungumza jambo
Msanii
 wa Bongo movie na aliyekuwa Jaji, Wema Sepetu akizungumza na mtoto 
aliyekuwa anashiriki kwenye shindano la kusaka vipaji kwa watoto wenye 
miaka minne mpaka miaka 14.
Baadi ya washiriki waliofika wakiwa na wazazi wao kwenye shindano la kusaka vipaji vya watoto wanaojua kuigiza.
Mmoja
 wa watoto akiigiza kwa kulia mbele ya majaji (hawapo Pichani) katika 
shindano la kusaka vipaji vya kuigiza lililofanyika leo kwenye viwanja 
vya leaders Club.

 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Post a Comment